MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO


1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo leo Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu .
2
Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga  Akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa migogogoro ya mipaka kati ya hifadhi za Taifa na wananchi inapatiwa ufumbuzi leo Bungeni Jijini Dodoma.
3
Mbunge wa kuteuliwa ( CCM) Mhe. Anne   Kilango Malecela akisisitiza kuhusu Serikali kuweka mikakati ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara katika jimbo la Same ili kusaidia kukza uzalishaji wa mazao ya biashasra leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu  Bungeni Jijini Dodoma leo.
4
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akitoa maelezo Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwalipa fidia askari na wapiganaji wanaoathirika wakati wanatekeleza majukumu ya kulinda usalama ndani na nje ya nchi kwenye vyombo vya Umoja wa Mataifa (UN) au SADC  leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
5
Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
6
Mbunge wa  Geita Mhe. Msukuma Joseph Kasheku akiuliza swali Bungeni leo Jijini Dodoma kuhusu ni lini Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) utawasilisha bajeti yake ya kuhudumia jamii katika Baraza la Madiwani wa Geita ili waweze kuangalia vipaumbele vyao na kuwapa vipaumbele vya Halmashauri hiyo.
7
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus  Nyongo akieleza mikakati ya Serikali kuwawezesha wachimbaji wadogo katika maeneo yote nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni