Waziri wa Madini Mhe. Angellah
Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya
Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge Uratibu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama akitoa maelezo Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na
Serikali katika kuwalinda watoto wa kike ambapo ameahidi kuwa Serikali
itatoa taarifa rasmi kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowadhalilisha
kijinsia watoto wa kike na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya
Serikali kupambana na Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha
upimaji wa Virusi vya UKIMWI hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue
hali zao na kuchukua hatua stahiki.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama Jenerali Venance Mabeyo (wakwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya
Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.
Idrissa Kikula aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa Makamishna wa Tume
hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara baada ya
kipindi cha maswali na majibu.
Sehemu ya Viongozi wa Tume ya
Madini na wageni mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini
wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo.
Sehemu ya Wanafunzi waliofika
Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa
kipindi cha maswali na majibu.
( Picha zote na mahmoud ahmad)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni