Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Leodgar Tenga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo mchana wakati akitangaza rasmi \tarehe ya kutoa Tuzo za Rais za Viwanda zinazotarajia kufanyika Mei 4 mwaka katika Hoteli ya Serena, ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa CTI, Dkt. Samuel Nyantahe na Makamu wa pili wa Mwenyekiti CTI, Shabbir Zavery. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Na Leandra Gabriel, Mafoto Blog, Dar
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tuzo za Rais za Mzalishaji bora wa Viwandani (PMAYA) za mwaka 2017 zinazotarajiwa kufanyika Mei 4 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo la PMAYA zinazoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) hutoa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri katika mwaka uliopita likiwahusisha wanachama wa CTI na wasio wanachama.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam,mchana huu, Mkurugenzi mtendaji wa CIT Leodger Tenga amesema kuwa tarehe 7 Desemba mwaka jana walizindua shindano la mzalishaji bora wa kampuni na tayari kampuni 36 ziliweza kujitokeza kwenye mchakato huo ukiwa umeenda vizuri na washindi wamepatikana ambao watakabidhiwa zawadi zao siku hiyo ya ijumaa, Mei 4.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Machapisho wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Thomas Kimbunga, akitangaza utaratibu wa upatikanaji wa washiriki wa tuzo hizo,wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, ambao ni sehemu ya waratibu mkutano huo, Teddy Mapunda, akiongoza mkutano huo,
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Machapisho wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Thomas Kimbunga, akitangaza utaratibu wa upatikanaji wa washiriki wa tuzo hizo,wakati wa mkutano huo. kutoka (kushoto) ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Theresia Mmary, Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa CTI, Shabbir Zavery, Mwenyekiti wa CTI, Dkt. Samuel Nyantahe na Mkurugenzi Mtendaji, Leodgar Tenga.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Dkt. Samuel Nyantahe, akizungumza na waandhishi wa habari kuhusu tuzo hizo.
Kwa upande wa mwenyekiti wa shirikisho hilo Dkt. Samwel Nyantahe ameeleza kuwa shirikisho hilo ni la wamiliki wa viwanda nchini ni kwa lengo la kuweka mazingira ya uzalishaji nchini na shindano hilo linatoa nafasi ya kutangaza bidhaa kwa wafanyabiashara na kupata nafasi ya kukutana na Rais na kuzungumza naye ikiwa ni muhimu kwa kuwa tunaelekea katika uchumi wa viwanda.
Mashindano hayo yanahusisha zaidi ya sekta 18 na makampuni 36 na kuna zawadi maalumu kwa washindi wa matumizi bora ya nishati katika viwanda vyao.
Mkurugenzi wa machapisho wa (CTI) Thomas Kimbunga ameeleza kuwa namna ya kushiriki ilikuwa katika makundi matatu ya viwanda yaani vile vikubwa, vidogo na vya kati na washiriki wameshindanishwa kulingana na makundi waliyoshindania na vigezo katika kila kundi ni pamoja na mazingira, mahusiano kazini na kuendeleza wafanyakazi sambamba na suala la ubora wa bidhaa kwa kuthibitishwa na TBS.
Aidha ameeleza kuwa shindano hilo litatasaidia kuongeza ufanisi hasa katika utendaji kazi katika sekta mbalimbali za viwanda pia washiriki watapata nafasi ya kujua maeneo waliyofanya vizuri na kupata nafasi ya kuboresha vyema bidhaa zao.Baadhi ya vigezo ambavyo vimezingatiwa ni pamoja na faida kwa jamii, afya na usalama, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, utendaji kiuchumi, utendaji kiteknolojia na matumizi bora ya nishati.
Sehemu ya wanahabari wakiwa bize kurekodi hotuba ya Mwenyekiti huyo.
Wanahabari wakiwa kazini.....
Baadhi ya wageni waalikwa katika mkutano huo....
Mwakilishi wa Hoteli ya Serena ambao ni moja kati ya wadhamini, Meneja wa mikutano na matukio, Alex Maboko, akizungumza jambo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni