Mbunge wa
Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amefagilia utendaji kazi wa Rais
John Magufuli kwamba amekuwa akitekeleza majukumu yake bila kubagua vyama vya
siasa, huku akitolea mfano jinsi fedha za miradi mbalimbali zinavyomiminika
jimboni kwake
Mchungaji
Msigwa ametoa kauli hiyo jana Mei 2, 2018 katika Ikulu ndogo ya Iringa kwenye
hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Rais Magufuli
Hata hivyo,
Msigwa Alipoulizwa kuhusu video inayosambaa ikionyesha akimwagia sifa kiongozi
mkuu huyo wa nchi, amesema ni kweli ila video hiyo imekatwa na kuna mambo
aliyoyazungumza, ikiwamo wanachama mbalimbali wanaohamia CCM
Wakati
akizungumza katika hafla hiyo Mchungaji Msigwa amesema, “Mheshimiwa Rais
umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa hujali vyama na hilo limekuwa
likidhihirika hujali vyama. Umesaidia sana bahati mbaya hawakukupangia ratiba
ya kufungua miradi, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi.”
“Amezungumza
Mahiga (Balozi Augustine-Waziri wa Mambo ya Nje) tuna barabara nzuri katika
kipindi chako ambacho umekuwa rais. Tumejenga barabara ya lami mradi wa Benki
ya Dunia kutoka Mlandege mpaka kwa mkuu wa wilaya karibu Sh3.5bilioni.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni