washtakiwa wa kosa la kutokua na vyoo wakiwa katika mahakama ya wilaya ya Longido
Wananchi 15 wakazi wa kijiji cha
Gebailumbwa wilaya ya Longido,Mkoani Arusha wamepandishwa kizimbani katika
mahakama ya wilaya hiyo wakikabiliwa na makosa matatu ya kutokuwa na vyoo
na kusababisha mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu.
Akisoma mashitaka hayo April 2 mwaka huu, mbele ya hakimu
mfawizi wa mahakama hiyo,Aziza Temu,Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi
wilayani hum
o,Anzulimu Mihella amesema kuwa,shtaka la kwanza na la
pili linawakabili washtakiwa wote kwa pamoja.
Washtakiwa hao ni Oleulei Losinigi(50),Kirusu Taitai(48),
Kelepu Kesonyi(35)Lazaro Parteye(38),Joshua Metui(20)Kamete Lemomo(25)Kimare
Lamama(38)Lemomo Kokoyo(25)na Zacharia Kabamngasi(33).Wengine ni Paulo Lemomo(30),Kaika Ngatete(55)Thimotheo
Kibangasi(37) na Moko Tataya(75)
Amesema mnamo mwaka 2016 na April 30 mwaka 2018 washtakiwa
hao kwa pamoja walitenda kosa kwa kukaidi Amri halali ya kuchimba vyoo ,jambo
ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 124 sura ya 16 ya mwaka
2009.
Washtakiwa hao waliokuwa wakiongozwa na mwanasheria
wao,Nicholaus Senteu walikana mashtaka na hakimu Temu alidai dhamana ipo wazi
kwa kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa Umma mwenye
kuweza kusaini bondi ya shilingi milioni 10 kila mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni