Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akisisitiza jambo mbele ya meza kuu na wageni wa alikwa, tukio
lililojiri katika viunga vya Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi
(TFDA).
Watumishi
wa umma na wageni waalikwa wakiwa wakifuatilia kwa ukaribu taarifa
iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu(MB) hayupo
kwenye picha, mapema katika uzinduzi wa Maabara hamishika uliofanyika
katika ofisi za TFDA.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara hamishika hizo,
wakwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa, watatu
kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya TFDA Bi. Zainabu na wa mwisho ni
Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Hiiti B. Sillo.
Mh.
Ummy Mwalimu akipata maelekezo kuhusu Maabara hamishika hiyo wakati wa
uzinduzi wa maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO
Dkt. Matthius Kamwa.
Meza
kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema
katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amesema kuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa ni Taasisi bora
kwa Bara la Afrikakatika kudhibiti dawa na chakula ili watanzania wapate
huduma bora.Ummy
ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Maabara Hamishika jijini Dar es
Salaam, amesema kuwa katika kulinda afya za wananchi ni kupata dawa
zinazostahili ambazo zimedhibitiwa na TFDA.Amesema
kuwa matumizi ya dawa zisizo sahihi zinarudisha kasi ya uchumi ambayo
inatokana na watu kuingia gharama za kununua dawa hizo mara kwa mara na
tatizo kubaki pale pale.
Ummy
amesema kuwa licha ya kudhibiti dawa lakini TFDA isiwe kikwazo cha
uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo wawekezaji wanatakiwa kufuata
taratibu za nchi zilizowekwa.
Aidha
amesema kuwa kazi ya TFDA ni kuhakikisha afya za wananchi zinalindwa
kwa kuwa na wananchi wenye afya njema na wanaweza kuwfanya kazi na
kuliletea Taifa maendeleo.
Amesema
TFDA inatakiwa kuzingatia tathimini ya kina ya kisanyasi pamoja na
matokeo ya uchunguzi wa maabara hivyo maabara ya TFDA ni kiungo muhimu
katika kutekeleza jukumu la kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa hizo.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema jukumu la TFDA ni
kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa wa bidhaa ya chakula na dawa,
vipodozi na vifaa tiba na vitandanishi ili kulinda afya ya jamii dhidi
ya madhara yanayoweza kutokana na matumizi ya bidhaa duni na bandia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni