KATIBU MTENDAJI BARAZA LA HABARI AWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUWAELEZA WAANDISHI SERA ZA VYOMBO VYAO


index
Baraza la habari Tanzania (MCT) limewataka wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari kuweka wazi sera na taratibu za vyombo hivyo kwa waandishi wao ili kuwaepusha na vikwazo ,usumbufu,na madhara pindi wawapo kwenye kazi zao.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bw.Kajubi Mukajanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga jinai dhidi ya wanahabari yaani(International Day to end impunity for crime Against journalists) ambapo amewataka wamiliki na wahariri kuziweka wazi sera za vyombo vyao ili kuwasaidia waandishi wao kujua nini wanatakiwa kukiandika au kukichapisha ili kisilete madhara na migogoro katika jamii kwakufanya hivo itasaidia kupunguza madhira wakiwa kazini.
Aidha Bw.Mukajanga amewakumbusha viongozi wa vyombo vya habari hususani wamiliki,watendaji wakuu na wahariri wajibu wao wa kuwalinda waandishi wao na kuzingatia usalama wao.
Hata hivyo Bw.Mukajanga  ameasa vyombo vya habari visipuuze sheria zilizopo kwani hata kama ni mbaya na ngumu kwa kiasi gani lakini zipo na zinaweza kufanyiwa kazi wakati wowote pia amesisitiza juhudi za pamoja ziimarishwe kuhakikisha kuwa sheria hizo mbaya zinafutwa au kufanyiwa marekebisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni