Na Mahmoud Ahmad Arusha
JESHI la polisi mkoa wa Arusha linamshikilia
mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA) kwa tuhuma za
kutoa na kusambaza maneno ya uchochezi katika mitamndao mbalimbali ya
kijamii.
Akithibitisha kukamatwa kwa mbunge Lema mbele ya vyombo vya habari kamanda wa
polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema Lema alikamatwa jana majira ya saa
12;00 asubuhi nyumbani kwake Njiro akiwa amelala.
Alisema baadhi ya menono hayo ni
“Kama mauti imepoteza utukufu wake hakuna statement ya kurudisha nyumba Arusha
kuandamana”
Kwa mujibu wa kamanda maneno hayo
aliyotoa Lema ni ya uchochezi na kuvuruga amani ya nchi na ndiyo maana
wanamshikilia kwa ajili ya mahojiano juu ya kaluli zake hizo
.
Alisema watanzania wanatambua
umuhimu wa amani na hakuna mtu aliyejuu ya sheria hivyo ni vyema tukaheshimu
amani na utulivu tulionao.
Aidha alisema utii wa sheria bila
shurti ni vyema ukazingatiwa ili kuepuka machafuko ambayo yanaweza kutokea
kutokana na maneno hayo ya uchochezi.
Hata hivyo polisi baada ya kumkamata wameifanyia upekuzi nyumba yake ili kubaini
iwapo kuna vitu vyenye kuashiria uchochezi zikiwemo fulana ama bendera zenye
maandishi ya Ukuta.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni