Na Mahmoud Ahmad Arusha
CHAMA cha Mapinduzi ,CCM, mkoa wa Arusha, kimepiga marufuku
makundi yote ndani ya chama ambayo
yalikuwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kukipatia ushindi chama cha
mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2015.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, wa ccm, mkoa wa Arusha, Shaban
Mdoe, amesema chama cha mapinduzi kwenye kikao chake cha kamati ya Siasa ya
halmashauri kuu ya mkoa, imepiga marufuku makundi hayo kuanzia Augosti 22 mwaka
huu .
Amesema baada ya kamati
ya siasa kuridhika kuwa kwa sasa makundi hayo hayana tija na kuendelea kuwepo
yataleta mgawanyiko ndani ya chama hivyo kimeazimia makundi yote yavunjike na kubakia kundi moja
tu la chama cha mapinduzi..
Amesema miongoni mwa makundi hayo ni lile linalojiita Team
Magufuli, na Club Magufuli, Chama cha mapinduzi kilitumia mbinu mbalimbali za
kuwafikia wapiga kura ikiwemo kwenye mikutano
ya kampeni kupitia Chama na
jumuia zake pam,oja na mitandao ya
kijamii .
Amesema kwa siku za hivi karibuni kumeibuka tena kwa kundi linalojiita Team Magufuli na kufanya shughuli mbalimbali bila kukihusisha Chama wala jumuia zake ambapo ni kinyume na taratibu na kundi hilo halitambuliki tena na
chama kwa kuwa lililokuwepo lilishafutika baada ya uchaguzi kumalizika.
Mdoe, amesema kutokana na hali hiyo Chama cha Mapinduzi,
kinatoa onyo kwa watu wanaoanzisha makundi ya namna hiyo kwa jina la Chama pasipo
idhini na kufanya mambo nje ya utaratibu
kuacha mara moja.
Amesema Chama cha mapinduzi hakitasita kuwachukulia hatua za
kisheria wale wote watakaoanzisha makundi mengine .
.Mdoe, amesema mara baada ya uchaguzi mkuu kumalizika ccm mkoa
wa Arusha haina makundi ya wanachama bali ina kundi moja tu la CCM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni