Mkurugenzi
wa DOT Tanzania, Dawson Luogard akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa
maadhimisho ya siku ya vijana leo katika ukumbi FES Oyster Bay jijini
Dar es Salaam.
Mtandao
wa Vijana wa Activista Tanzania wakishirikiana na Tanzania Youth Vision
Association(TYVA) wameadhimisha siku ya Vijana Duniani kwa
kuwakutanisha vijana zaidi ya 120 kutoka maeneo mbalimbali na kujadili
mada mbalimbali kuhusu Kodi, Kilimo na Maendeleo Endelevu ya malengo ya
millenia.(Picha na Geofrey Adroph)
Mkurugenzi
wa Jielimishe Kwanza, Henry Kazure akitoa mafunzo kwa vijana waliofika
katika maadhimisho ya siku ya vijana katika ukumbi wa FES yaliyoandaliwa
na Activista Tanzania wakishirikiana na TYVA.
Katibu
wa Actvista Tanzania, Maria Kayombo ambaye alikuwa mshereheshaji
akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya vijana yaliyofanyika
katika ukumbi wa FES Oyster Bay jijini Dar es Salaam
Baadhi ya vijana wakifuatilia mada
Mratibu
wa Kwanza wa Activista Tanzania, Elly Ahimidiwe akizungumza na vijana
waliofika katika maadhimisho ya siku ya vijana yaliyoandaliwa na Mtandao
wa vijana wa Activista Tanzania wakishirikiana na TYVA.
Baadhi
ya Vijana waliofika katika maadhimisho ya siku ya Vijana wakisikiliza
mada zinazoendelea katika ukumbi wa FES Oster Bay jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Activista Tanzania, Hatibu Kilenga akifunga mafunzo kwa vijana yaliyoandaliwa na Mtandao
wa Vijana wa Activista Tanzania wakishirikiana na Tanzania Youth Vision
Association(TYVA) katika maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani.
Picha ya Pamoja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni