SAED Kubenea Mbunge wa Jimbo la Ubungo jana alijisalimisha Kituo Kikuu
cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuhojiwa kabla ya kupewa
dhamana kufuatia tuhuma za kuandika makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi
kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.
Kubenea ambaye anadaiwa kufanya uchochezi kwa kuandika makala katika
gazeti la MwanaHALISI toleo la 349 la Julai 25-31 yenye kichwa cha
habari, ‘Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?’
Kubenea alifika katika kituo hicho cha Polisi jana saa saba na robo
mchana (13:15) akiwa na Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Frederick Kihwelu wakili
mwandamizi wa Chama hicho.
Baaada ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa mawili, saa tisa na robo alasiri
(15:45) alitoka na kuondoka huku wandishi wa habari wakishindwa
kuzungumza naye baada Jeshi la Polisi kuwazuia waandishi wa habari
kuingia katika eneo la kituo hicho.
Akizungumza kwa njia ya simu, Lissu ambaye ndiye mwanasheria wa Kubenea
katika sakata hilo alisema kuwa, Kubenea amehojiwa kwa madai ya
uchochezi lakini alichokiandika ni hali halisi ya Zanzibar hususani
visiwa vya Pemba.
“Kubenea amechiwa kwa dhamana na ameamriwa kurudi tena kituoni hapo tarehe 18 Agosti, mwaka huu,” alisema Lissu.
Katika makala yake inayodaiwa kuwa ni ya kichochezi iliyokuwa na kichwa
cha habari, “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?” Kubenea alielezea jinsi
Jeshi Polisi Visiwani Pemba wavyonadaiwa kuwabambikia kesi wananchi,
kuwapiga na kuwatesa kwa madai kuwa wananchi hao wanaipinga serikali.
Kubenea aliandika Makala hiyo baada ya kusafiri kutoka Dar es Salaam
Mpaka Zanzibar kufuatilia kile alichokitaja kama mateso, unyanyasaji na
ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wananchi wasio na hatia visiwani
humo.
Miongoni mwa vijana na wahanga wa kubambikiwa kesi, kupigwa na kuteswa
visiwani Pemba waliotajwa na Kubenea katika makala yake ni ni Hijja
Hassani aliyetangazwa kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani kabla ya
Jecha Salim Jecha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta
uchaguzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni