TANZANIA YANDELEA KUTESA MASHINDANO YA MAJESHI AFRIKA MASHARIK

SE1
Nyota wa Mpira wa Pete wa Tanzania Mwanaidi Hassan (GS) akiwa katika hekaheka za kuisaidia Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki inayoendelea katika Uwanja wa Amahoro Kigali ambapo katika Mchezo huo Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
SE2
Nyota Chipukizi wa  Mpira wa Pete wa Tanzania Nasra Suleiman ( Mwenye  Mpira)akiwa katika hekaheka za kuisaidia Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
SE3
Kocha wa Timu ya Tanzania kwa Mpira wa Pete Argentina Daudi akitoa maelekezo kwa Wachezaji wake katika muda wa mapunziko katika mchezo baina yao na Rwanda  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali  ambapo Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
SE4
Mlinzi wa Timu ya Mpira wa Pete wa Tanzania Joyce Kaira (GK) akiwa katika hekaheka za kuzuia Wachezaji wa Rwanda  Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo katika Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Amahoro  Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
SE5
Mchezaji wa Mpira wa Pete wa Tanzania Nasra Suleiman ( GA)akiwa katika harakati za kuifunia Timu yake katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali  ambapo katika Mchezo huo Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
SE6
Mchezaji wa Mpira wa Pete wa Tanzania Nasra Suleiman ( GA)akiwa katika hekaheka za kuisaidia Timu yake kupata Ushindi katika mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki yanayoendelea katika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo katika Mchezo huo Tanzania iliifunga Rwanda 56-13(Picha na Dora Mushi) .
SE7
Kikosi cha Mpira wa Miguu cha jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja Muda mfupi kabla ya Kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Kenya uliofanyika katika Uwanja wa  Nyamirambo Rwanda ambapo Tanzania iliibuka na Ushindi wa Bao 2-1.
……………………………………………………………………………………
Na Selemani Semunyu JWTZ
Timu ya Mpira wa Pete ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imedhihirisha Ubabe wake katika mchezo huo baada ya kuifunga Timu ya Jeshi la Rwanda RDF kwa Magoli 56-13 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na Timu zote tangu kuanza Mashindano hayo.
Tangu Mwanzo wa Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Rwanda walionekana kuzidiwa na kiwango kilichoonyeshwa na Tanzania kupitia Nyota wake Mwanaidi Hassan aliyefunga 37 na Nasra Suleiman aliyefunga 19 waliokuwa mwiba kwa Timu ya Rwanda kutokana na kupachika magoli kila wapatapo mpira.
Tanzania iliweza kumiliki vipindi vyote vine vya mchezo huku Rwanda wakionekana kutoelewana kutokana na idadi ya magoli waliokuwa wakifungwa tangu Robo ya Kwanza mbayo ilimalizika kwa Tanzania kuongoza kwa 13-2 huku Robo ya pili 32-6 na Robo ya tatu 42-10.
Kwa upande wake Mchezaji Nasra Suleiman alisema mbali na kupata ushindi huo lakini hawatobweteka kwani wanawasubiri Kenya ili kutangaza Ubingwa kwa kushinda Michezo yote.
Kwa upande mwingine Tim u ya Mpira wa Miguu ya Tanzania wameinyamazisha Timu ya Jeshi ya Kenya baada ya kuwafunga mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Kigali Nyamirambo.
Katika Mchezo huo Kenya Ndio walianza kupata bao  Muda mchache kabla kwenda mapumziko katika Dakika ya 42 kupitia kwa mchezaji wake  Private Peter Onyango  kabla ya Dakika tatu Baadae Private Prosper  Mkwama kusawazisha bao na kwenda mapumziko wakiwa Sare.;
Kipindi cha Pili kilianza huku Timu zote zikifanya mabadiliko na kosa kosa ya magoli kwa Nyakati tofauti lakini Mnamo dakika ya 77 Private Abdulrahman Musa akaiandikia Tanzania bao la Pili na la ushindi.
Kufuiatia matokeo hayo sasa Tanzania wamebakiza Mchezo mmoja na Rwanda utakaopigwa siku ya ufungaji  Agosti 17 katika Uwanja wa Amahoro huku Timu ya mpira wa Pete wanatarajia kukutana na Kenya Agosti 14

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni