UTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007). Takribani kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi  katika kupata huduma za afya.
Wasimamizi wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. Mhe Waziri amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.
Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: waziri@moh.go.tz

“Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.



MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)


NA.
MKOA
JINA LA MGANGA MKUU
NAMBA YA SIMU
NUKUSHI
1.
ARUSHA
DKT. FRIDA MOKITI
0784-264750
fridamokiti@yahoo.com.
2.
DAR ES SALAAM
DKT. GRACE MAGEMBE
0767-300234
magembegrace@yahoo.com
3.
DODOMA
DKT. JAMES CHALRES
0784-504955
jcrexford@yahoo.com
4.
IRINGA
DKT. ROBERT M. SALIM
0754-377176
saludimwe@yahoo.com
5.
KAGERA
DKT. THOMAS RUTACHUNZIBWA
0754-803729
thomasruta@yahoo.com
6.
KIGOMA
DKT. PAUL CHAOTE
0755-696855
pchaote@gmail.com
7.
KILIMANJARO
DKT. BEST MAGOMA
0754-621046
8.
LINDI
DKT. SONDA YUSUPH
0653-384350
sonda_y@yahoo.com
9.
MANYARA
DKT. SUNGWA KABISSI NDAGABWENE
0713-450765
Mas19730ok@yahoo.co.uk
10.
MARA
DKT. SAMSON WINANI
0784-450425
sam.winani@yahoo.co.uk
11.
MBEYA
DKT. SEIF MHINA
0767-832275
sbmhina@gmail.com
12.
MOROGORO
DKT. JACOB FRANK
0767-985850
13.
MTWARA
DKT. WEDSON SICHALWE
0755-048787
14.
MWANZA
DKT. LEONARD SUBI
0784-501020
subileon@yahoo.com
15.
PWANI
DKT. BEATRICE BYARUGABA
0784-319764
bykami@yahoo.com
16.
RUKWA
DKT. JOHN GURISHA
0784-216008
igurisha@yahoo.com
17.
RUVUMA
DKT. DAMAS KAYERA
0713-537495
dajkay@gmail.com
18.
SHINYANGA
DKT. NTULI KAPOLOGWE
0654-586346
nkapologwe2002@gmail.com
19.
SIMIYU
DKT. MAGEDA KIHULYA
0754-507875
mkihulya@yahoo.com
20.
SINGIDA
DKT. JOHN MWOMBEKI
0786-103225
johnmwombeki@yahoo.co.uk
21.
TABORA
DKT. GUNINI KAMBA
0783-344079
gunini@yahoo.com
22.
TANGA
DKT. ASHA MAHITA
0715-465521
ashamahita@yahoo.co.uk
23.
GEITA
DKT. JOSEPH KISALA
0788-046787
joskisala@gmail.com
24.
KATAVI
DKT. YAHYA HUSSEIN
0754-372772
hyahaya70yahoo.com
25.
NJOMBE
DKT. SAMUEL MGEMA
0757-226806
mgemasamuel@gmail.com



IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni