TAARIFA KWA UMMA
Klabu
ya Simba inapenda kutoa taarifa kwa wanachama,wapenzi wake na washabiki
wa mchezo wa mpira wa miguu kote nchini kuwa tamasha la kila mwaka la
klabu yetu linalojulikana kwa umaarufu wa Simba Day lipo pale pale na
wala 'halijapeperushwa' kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya
habari nchini.
Ni
upotoshaji mkubwa usiozingatia weledi na maadili ya taaluma
kulikopitiliza kulikofanywa na chombo hicho ambao unaweza kuleta athari
kubwa kwa tamasha letu ambalo ni sehemu ya sherehe muhimu ya kuadhimisha
miaka themanini toka kuanzishwa kwa klabu yetu yenye historia ya
kutukuka ndani na nje ya mipaka yetu kupita klabu yoyote nchini.
Katika ratiba ya tamasha letu hili kesho kutakuwa na shughuli ya usafi
kwenye mtaa wa Msimbazi yalipo makao makuu ya klabu na shughuli hii
itaanza saa mbili kamili asububi na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mbunge
wa jimbo la Ilala yalipo makazi ya klabu Mh Mussa Azzan Zungu.
Tunawaomba
wana Simba wote mjumuike kwenye jambo hili muhimu ambalo pia ni maagizo
ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Mh John Pombe Magufuli.Pia
hiyo kesho Jumamosi ya tarehe 6-8-2016 itakuwa ni siku ya kupiga picha
za msimu kwa wachezaji na benchi zima la ufundi la klabu ya
Simba.Jumapili ya tarehe 7 ni siku ya wachezaji na benchi la ufundi kuwa
live mitandaoni kwa kuperuzi na wana Simba kuhusina na masuala mbali
mbali.
Sambamba na mkutano na wanahabari kati ya makocha na manahodha wa klabu ya AFC Leopard ya Kenya na sisi wenyeji wao Simba SC.
Kilele
cha sherehe zenyewe ni siku ya Jumatatu tarehe nane mwezi huu pale
uwanja wa Taifa hapa jijini kutakapokuwa na mechi kabambe baina yetu na
Leopards.
Mbali
ya mechi hiyo ambayo itawatambulisha wachezaji wote wa msimu huu wa
Simba pamoja na mchezaji Laudert Mavugo ambae tayari yupo kambini.Pia
kutakuwa na burudani mbali mbali za muziki na sanaa
Siku ya kilele viongozi mbali mbali watahudhuria huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda.
Sanjari na viongozi hao, viongozi wote wa Simba wakiongozwa na Rais wa
klabu Evans Aveva watashiriki kiukamilifu shughuli zote za tamasha hili
kubwa kupita lolote linalohusisha vilabu vya soka kwenye ukanda huu wa
Afrika Mashariki.Niwajulishe tu viongozi wetu wanaendelea na shughuli
zao kama kawaida huku tukiwaachia vyombo vya uchunguzi vikiendelea na
kazi zao.
Klabu haitaki kuingilia kwa namna yoyote ile
uchunguzi wa Takukuru na inaamini itajiridhisha na nia 'NJEMA' ya kamati
ya utendaji ya klabu ya Simba.
Mwisho ingawa sio kwa umuhimu
nitumie fursa hii pia kuwashukuru watanzania wote kwa dua na sala zao
kwangu binafsi kwa kupata maradhi ya macho ambayo kwa kiwango kikubwa
sana yamenusurika kwa jitihada za madaktari wa Tanzania na nchini India.
Jitihada zao zilikubaliwa na Mwenyezi Mungu ambae bila shaka alizikubali dua na sala zenu
Asanteni sana watanzania wenzangu.
Imetolewa na
HAJI S.MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SPORTS CLUB
SIMBA NGUVU MOJA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni