Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amefungua rasmi mashindano ya soka ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya na
kuvitaka vilabu vya soka kutumia vipaji vinavyoibuliwa na programu hiyo
ya vijana. Ufunguzi huo ulifanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya leo Agosti 9, 2016.
“Hii
ndio njia pekee ambayo inaweza kutuletea maendeelo ya soka na kuiwezesha
nchi yetu kuondokana na matokeo mabaya katika mashindano mbali mbali ya
kimataifa”, alisema. Aliishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kubuni
programu hii ambayo imekuwa ikiwapa vijana fursa ya kuonyesha na
kuviendeleza vipaji vyao.
Makala
amewataka vijana kucheza kwa kujituma na kufahamu kwamba hatma ya
mchezo wa soka hapa nchini iko mikononi mwao. Alilitaka Shirikisho la
soka nchini (TFF) kufanya kazi kwa karibu na wadau wengine ili
kuhakikisha kuwa vijana wanaoibuliwa kupitia Airtel Rising Stars
wanaendelezwa.
Amewataka
viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya (MREFA) kuyatumia vizuri
mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa na kuchagua vijana nyota
watakaounda timu za mkoa kushiriki kwenye fainali za Taifa za Airtel
Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 6
hadi 11 jijini Dar es Salaam.
Michuano
ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa inaendelea katika mikoa minginge
ambapo timu za wavulana za Makongo Sekondari na Kawe United zilitoshana
nguvu baada ya kutoka suluhu katika uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe,
jijini Dar es Salaam.
Fainali
za Taifa zitashirikisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya
kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Timu nyingine zitatoka Morogoro,
Mwanza, Mbeya, Arusha, Lindi na Zanzibar.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya,Amoss Makalla aliye simama akizungumza na wachezaji
kabla ya kuzindua michuano ya Airtel Rising Star kwa Mkoa wa Mbeya iliyo
anza kutumia vumba jana katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na
kushirikisha timu sita.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akisalimiana na wachezaji wa timu ya Dable
'A' ya jijini Mbeya kabla ya kuzindua rasmi michuano ya Airtel Rising
Star Mkoa wa Mbeya iliyoanza jana katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
kwa kushirika timu sita za vijana.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akisalimia na mchezaji Alvira Zaibu wa
tatu kushoto, kutoka timu ya soka ya watoto ya Mbeya Talent wakati wa
ufunguzi wa Michuano ya Airtel Rising Star iliyonza kutimua vumbi jana
katika dimba la Sokoine kwa kushirikisha timu sita za Mkoa Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipiga mpira golkini ishara ya ufgunguzi
rasmi ya michano ya mpira wa miguu kwa vijana chini miaka 17 Airtel
Rising Stara iliyonza jana katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akifatalia mchezo wa ufunguzi wa michuano
ya vijana chini ya miaka 17 Airtel Risin Star kati ya Mbaspo Academy
dhidi ya Dable A zote kutoka jijini Mbeya uliomazika kwa Mbaspo kuibka
na ushindi wa bao 4-0 ndani ya Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Afisa
Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa
Airtel Mkoani Mbeya wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising
Stars mkoani hapo
Wachezaji
kutoka timu sita zinazo shiriki Michuano ya Airtel Rising Star chini ya
miaka 17 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amsos Makalla hayupo
katika picha kabla ya kuzindua rasmi michuano hiyo kimkoa jana katika
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni