Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 
16 Agosti, 2016 amewatembelea na kuwajulia hali Spika wa Bunge la 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Makamu wa Rais 
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. 
John Samuel Malecela Jijini Dar es Salaam.
Pamoja
 na kuwajulia hali, Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth 
Magufuli amewaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone na kupata nguvu haraka ili
 waweze kuendelea na majukumu yao ya kawaida katika ujenzi wa 
Taifa.Akizungumza na Rais Magufuli nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es
 Salaam spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemshukuru Rais Magufuli kwa 
kumtembelea, kumjulia hali na kufuatilia kwa ukaribu wakati wote 
alipokuwa akipata matibabu nchini India hadi aliporejea hapa nchini.
"Kwa
 kweli nimefarijika sana, kwanza naomba nimshukuru sana Mhe. Rais kwa 
sababu nilipopata matatizo haya ya maradhi alikuwa karibu sana na mimi 
nikiwa hapa nchini na hata nilipopelekwa nchini India alinipigia simu 
mara kwa mara na kunifariji sana, na hapa amekuja kuniona kwa niaba ya 
watanzania kwa kweli namshukuru sana na namuombea kwa Mwenyezi Mungu 
aendelee kumpa moyo huu wa kuwajulia hali wale wenye matatizo 
mbalimbali"Lakini
 niwahakikishie Watanzania, kwamba kwa sasa nina nafuu kubwa sana, 
naweza kufanya kazi nyingi tu sasa lakini tuendelee kuombeana" Ameeleza Mhe. Ndugai alipokuwa akizungumzia hali yake kwa sasa.
Kwa
 upande wake Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John 
Samuel Malecela pamoja na kumshukuru Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth 
Magufuli kwa kumtembelea amesema afya yake inazidi kuimarika na pia 
amewashukuru Madaktari wanaompatia matibabu.
"Mheshimiwa
 Rais nakushukuru sana, namshukuru pia Mama Janeth Magufuli kwa 
kunitembelea na kunifariji, naendelea vizuri na matibabu na afya yangu 
imeimarika kwa kiasi kikubwa" Ameeleza Mhe. Malecela.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
16 Agosti, 2016.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
 jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai 
nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia 
hali. 
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na 
Mke wake Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala 
sala jijini Dar es Salaam walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa 
Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.
 Mke
 wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Spika wa Bunge la Jamhuri
 ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwa 
Spika Sala sala jijini Dar es Salaam. 
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia 
hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu 
jijini Dar es Salaam. 
 Mke
 wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu mstaafu John 
Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam. 

 Mke
 wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe 
Magufuli akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel 
Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango Malecela.
 Mke
 wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Mke wa Spika Dkt. Fatma 
Mganga Ndugai wakati alipokwenda na Rais Dkt. John Pombe Magufuli 
kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU








Hakuna maoni:
Chapisha Maoni