Na Mahmoud
Ahmad Arusha
Wakazi wa
Kitongoji cha Shimbumbu Kata ya Ngwarusambo wilayani Meru wameimbo serikali
kuitupia macho Kero yao ya Maji safi inayowasumbua kwa mda sasa licha ya fedha
za Ahadi ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kutoa fedha hizo kiasi cha million
50 za uwekaji wa mabomba katika eneo hilo.
Akizungumza
na wanahabari kijijini hapo Mwenyekiti wa kitongoji hicho Michael Mungure
alisema kuwa wananchi wa kijiji cha Kimundo wamekuwa wakitaabika na adha ya
maji kwa muda mrefu sasa ambapo mabomba ya mradi yamefika nusu badala ya
kumalizia mradi huo kwa mda sasa.
Alisema kuwa
mabomba ya maji ya kueneza maji maeneo mbali mbali katika kata yao yamefika
nusu hali inayopelekea wananchi kuapata adha kubwa ya kuacha shughuli za
maendeleo na kutafuta maji.
“Mh.Kinana
alitoa ahadi ya kukamilisha kwa fedha kiasi cha million 50 hadi leo fedha za
ahadi hazijatumika ipasavyo kukamilisha mradi kusudiawa na wananchi kupata maji”alisema
Mungure
Aliwataka
viongozi wa wilaya hiyo akiwemo mkurugenzi mpya wa halmashauri ya Meru na
diwani wa kata Jeremia Kanuya kutembelea eneo hilo na kuibua kero mbali mbali katika
wilaya hiyo ikiwemo uchimbaji wa mawe katika maeneo ya kitongoji hicho mradi
ambao umekuwa ukisaidia wananchi kupata fedha za kujikimu kimaisha na kupunguza
tatizo la ajira.
Aidha alitoa
wito kwa Serikali badala ya kuzui mradi wa uchimbaji mawe ukaibua fursa
nyingine za wananchi kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.
Akalitaka
jeshi la polisi kufika vijijini na kutoa elimi kwa Polisi jamii wanaolinda
maeneo yao kwani wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na vile vile
kushirikiana na wenyeviti Vijiji,watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vitongoji
katika suala zima la ulinzi shirikishi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni