MWANARIADHA WA BAHAMA ASHINDA MEDALI DHAHABU BAADA YA KUJIRUSHA NA KUMALIZA MBIO

Mwanariadha wa kike wa Marekani, Allyson Felix, alionekana kukaribia kushinda mbio za mita 400 hata hivyo alijikuta akizidiwa maarifa na Shaunae Miller wa Bahama ambaye alijirusha na kushinda.

Baada ya mbio hizo ilimchukua Felix karibu saa moja kuweza kupata nguvu ya kuongea na waandishi wa habari, na kuwaambia amefadhaika kwa kushindwa kushinda medali ya dhahabu kwa taifa lake la Marekani.
    Shaunae Miller akijirusha na kumaliza mbio hizo kwa ushindi na kumshinda    Allyson Felix
Picha ikionyesha mikono ya Shaunae Miller ikiwa imekatiza katika mstari wa kumalizia mbio huku mkuu wa kulia wa Allyson ukiwa ndio unakanyaga mstari huo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni