| Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo akihutubia wageni katika hafla hiyo | 
| Meza Kuu ambapo wageni rasmi waliketi katika hafla hiyo | 
| Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akizungumza wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo | 
| Kutoka kushoto ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini Mh.Felix Mrema, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko BRITAM Kenya na mwisho ni Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera | 
| Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa Kampuni hiyo mbele ya wageni waliohudhuria katika hafla hiyo | 
| Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru | 
| Mbunge wa Arusha Mjini Mh.Godbless Lema pamoja na mke wake wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika hafla hiyo ndani ya Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha | 
| Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera akimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati akihutubia wageni katika hafla hiyo | 
Habari Mahmoud Ahmad,Arusha.
Kampuni
 ya Bima ya Britam imeadhimisha miaka 50 ya kutoa huduma za bima nchini 
Tanzania huku ikiongoza katika utoaji wa huduma bora za bima za 
magari,nyumba ,mali pamoja na afya.
Sherehe
 za Maadhimisho hayo zimefanyika katika Hotel ya Mount Meru iliyoko 
jijini Arusha na kuudhuriwa na Viongozi wa kiserikali pamoja na Wadau wa
 Bima.
Afisa
 Mkuu wa  Kampuni hiyo  nchini Tanzania  Stephen Lokonyo amesema kuwa 
kampuni hiyo imejipanga vizuri kuwahudumia watanzania na kuwafikia watu 
wengi zaidi ili waweze kunufaika na huduma za bima .
Aliongeza
 kuwa wao kama kampuni ya bima ya Britam wamejipanga kuwasaidia wananchi
 mbalimbali wakiwemo wa juu pamoja na wachini kwakuanzisha bima za aina 
mbalimbali ikiwemo ya mali zao kama nyumba ,bima za afya pamoja bima ya 
kilimo kwa ajili ya wakulima pamoja na wafugaji.
Mkuu
 wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliwataka mashirika ya bima 
kuwafikiria pia madereva bodaboda kwa kuwaanzishia bima za afya pamoja 
na bima za vyombo vyao ili pale wanapopata matatizo kama ya kuunguliwa 
na piki piki zao pamoja na kupata ajali waweze kusaidika kwa uraisi matibabu na kufidiwa pindi wanapopata ajali.
Alisema
 kuwa kumekuwa na pikipiki nyingi sana hivyo iwapo wataanzisha bima kwa 
ajili ya pikipiki wataweza kuwasaidia sana vijana pia wataweza kupata 
wateja wengi waotumia vyombo hivi.
Aidha
 mkuu huyo wa wilaya alihiasa  kampuni ya bima ya  Britam pamoja na 
kampuni zingine za bima kujikita  zaidi  kwa watu wenye kipato cha 
chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni