Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Old East International Moses Mwano akiwa anazungumza
na wateja waliotembelea banda hilo katika Maonyesho yanayoendelea
katika Viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.
Afisa
Mauzo wa Kampuni ya Old East International Vivian Stephano akiwa
anachukua kumbukumbu ya mteja Katika maonyesho yanayoendelea kwenye
viwanja vya Taso Njiro Jijini Arusha.
Meneja
mauzo wa Kampuni Old East International akiwa anamfafanulia mteja juu
ya Crown Cartridge,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya
Taso nanenane.
Afisa
Mipango wa Kampuni Old East International Ephrahim Moses Mwano akiwa
anaonyesha Aina ya Wino wa Crown ambao wanatengeneza hapa nchini,Katika
maonyesho ya wakulima na wafugaji Katika viwanja vya nanenane Njiro
Jijini Arusha.
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Wito umetolewa kwa Watanzania watumie na kuthamini bidhaa
zinazotengenezwa na kupatikana ndani ya nchi badala ya kuzipa kipaumbele
bidhaa za nje ya nchi.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Old East International
ndugu Moses Mwano ,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya
Taso nanenane njiro Jijini Arusha.
Mwao amesema kuwa Watanzania wengi wanathamini bidhaa
zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi,ambazo baadhi hazina kiwango cha
ubora unaotakiwa kwa mtumiaji.
Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Old East International
amesema kuwa kampuni hiyo ni ya Kitanzania ,imesajiliwa na ipo chini ya
Shirika la uwekezaji Tanzania wao ni wawekezaji wa ndani,wanahusika
kutengeneza wino wa kuchapia unaofahamika kwa jina la Crown Cartridge.
Kwa upande wake Mwano amewataka Watanzania kumuunga mkono
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dokta John Magufuli,katika jitihada zake za
kuifanya Nchi kuwa ya Viwanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni