Muswada binafsi wenye lengo la kutungwa kwa sheria ya kuwalinda albino umewasilishwa kwenye kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda.Muswada huo umewasilishwa bungeni na Mheshimiwa Shyrose Bhanji, mbunge wa Tanzania.
Katika muswada huo, Bhanji ameelekeza haki za msingi zinazopaswa kutolewa kwa walemavu hao kutoka Serikalini, Taasisi binafsi na kwenye jamii zetu.
Muswada huo kama utapitishwa na Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye Ualbino.
Muswada huo kama utapitishwa na Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye Ualbino.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni