Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tamisemi
mhe,George Boniface Simbachawene
Na. , Arusha.
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaagiza
maafisa utumishi kuwa waadilifu na wakweli katika kutunza nyaraka
zinazowahusu watumishi wenzao.
Aidha
serikali inatambua
kuwa inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii na inajitahidi kulipa madeni
hayo inayodaiwa na mifuko ya Hifadhi za Jamii .
Simbachawene
amesema hayo wakati akifungua mkutano wa tisa wa Mfuko wa Pensheni
wa LAPF kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Amesema
baadhi ya maafisa utumishi wamekuwa kama miungu watu na kupoteza
nyaraka za watumishi huku wanapobanwa na waajiriwa kuhusu taarifa za
watumishi husema uongo wakijua wenzao wanafamilia kama wao.
Pia
amekemea tabia ya watumishi wa masijala ambao wanapoteza kumbukumbu za
watumishi kwa makusudi hali inayosababisha baadhi yao kupunjwa madai yao
kutokana na baadhi ya kumbukumbu kupotezwa.
"Nawaomba
nyie maafisa utumishi muwe makini sana na maisha ya watumishi wenzenu
oneni huruma kwao mnapoteza kumbukumbu au kutoa ruhusa kwa watumishi
halafu mkibanwa mnasema hamna taarifa hii inawaumiza watumishi wenzenu
maana wanafamilia zao kwanini muwafanyie mambo yasiyofaa mjirekebishe
nyie pamoja na watu wa masijala ".
Naye Mwenyekiti wa
Bodi ya Mfuko wa Lapf, Profesa Faustine Bee amesema kuwa mfuko huo
unajitahidi kutoa huduma kwa wakati ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama
na kubuni mbinu za kukuza uchumi katika sekta ya viwanda.
Alisema
mfuko huo utaendelea kutoa huduma kwa wakati akiwemo fao la kulipwa
jana kwa wanachama wastaafu sanjari na kutoa mkopo wa maisha popote
unaotolewa kwa waajiriwa wapya kwakushirikiana na Benki ya CRDB.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni