WANAFUNZI WAPONDA RAHA FUKWE ZA MIAMI NA KUSABABISHA USUMBUFU


Polisi katika pwani ya Miami wanakabiliana hali ngumu ya kudhibiti usalama dhidi ya maelfu ya wanafunzi wa vyuo waliojaa kwenye Ufukwe wa Kusini baada ya kumalizika majira ya kipupwe.

Wanafunzi hao wamekuwa wakijirusha kwa kunywa pombe, kucheza huku wakisababisha uchafu mkubwa kwa kutupa chupa pamoja na taka nyingine nyingi katika fukwe hiyo hali inayochangia uharibifu wa mazingira.

Katika maeneo yote ya fukwe nchini Marekani maafisa wa majiji wanawakati mgumu katika kipindi hiki ambacho watu hufanyasherehe kwa wiki kadhaa wakiwa kwenye fukwe wakinywa pombe, kucheza na kufanya mambo mengine yasiyoyakistaarabu.
Polisi walio kwenye pikipiki za magurudumu manne wakijaribu kudhibiti nidhamu ufukweni
Wanafunzi wakiwa wamepozi katika moja ya magari ya polisi wakipiga picha katika ufukwe huku Miami
Hali ya uchafuzi wa mazingita inavyoonekana kufuatia kuanza kwa sherehe hizo katika fukwe kadhaa Marekani
Polisi wakiwa katika jukumu la kujaribu kuimarisha usalama na utulivu katika fukwe ya Miami

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni