Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Serikali
 imeahidi kuendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa kushirikiana na 
vyombo vya habari ili kwa pamoja kuweza kuhamasisha, kuunda na kujenga 
nchi ya viwanda katika kuunga mkono azma ya Rais Mhe. John Pombe 
Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
Hayo 
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo Mhe. Nape 
Moses Nnauye alipokutana na wamiliki na watendaji waandamizi wa vyombo 
vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
 wakati wa mkutano huo Mhe. Nnauye amesema kuwa serikali na vyombo vya 
habari wakishirikiana na kuwa na lengo moja wataweza kuileta Tanzania 
pamoja na kuiweka katika mwelekeo ulio sahihi. 
“Tukiamua
 leo kila chombo cha habari kikawa na dawati maalumu linalozungumzia 
Tanzania ya viwanda kama ilivyo kwa madawati mengine ndani ya vyombo 
vyetu vya habari, na serikali ikaendelea kutoa hamasa za uanzilishwaji 
wa viwanda ambavyo vitasukumwa na dawati hilo maalumu la viwanda, 
tutaweza kutimiza ndoto yetu ya Tanzania ya Viwanda” amesema Mhe. Nnauye
Akizungumza
 wakati wa mkutano huo Bw. Francis Nanayi kutoka Kampuni ya Magazeti ya 
Mwananchi amesema kuwa ili vyombo vya habari viweze kutangaza habari 
vinahitaji kupata ushirikiano wa kutosha kutoka serikalini kuonyesha 
mikakati na malengo ya serikali kuwezesha vyombo vya habari kujenga 
Tanzania ya viwanda na kuwapa fursa wananchi kupata taarifa sahihi za 
nchi. 
Naye 
Mtendaji kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Bibi. Mabe Masasi
 amesema kuwa Mapinduzi ya viwanda yanaweza kufanyika kama vyombo vya 
habari vitatoa taarifa sahihi za upatikanaji wa malighafi za uwekezaji 
kulingana na mahitaji yaliyopo katika maeneo husika na kuwekeza katika 
viwanda vidogovidogo vitakavyozalisha viwanda vikubwa.
Kwa 
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassani Abbas amesema 
kuwa atahakikisha maafisa habari wa serikali hususani maafisa 
wanaohusika na Sekta ya viwanda wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa 
vyombo vya habari ili kuweza kuelimisha umma namna Tanzania ya Viwanda 
inavyojengwa.
 Waziri
 wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) 
akiongea na wamiliki wa vyombo vya Habari (hawapo katika picha) wakati 
wa mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari 
vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda 
leo Jijini Dar es Salaam. katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. 
Elisante Ole Gabriel na kushoto ni  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas akitoa ufafanuzi kwa wamiliki wa vyombo vya habari namna uratibu wa matangazo utakavyokuwa ukiendeshwa na Serikali wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze leo Jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa vyombo vya Habari nchini kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya viwanda. Wanaomsikiliza kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na . Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas
Mkurugenzi wa Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akichangia wakati wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo vya Habari ikiwa ni muenedelezo wa vipindi vya Wadau Tuzungumze kinachoratibiwa na Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lengo likiwa ni kuimarisha ushirikaiano baina ya Wizara na wadau wa sekta zake.
 Mdau wa Habari Bw. Hamza Kasongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo 
Baadhi ya Wadau waliohudhuria mkutano
 wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki 
katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar 
es Salaam.
PICHA NA MICHUZI JR.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas akitoa ufafanuzi kwa wamiliki wa vyombo vya habari namna uratibu wa matangazo utakavyokuwa ukiendeshwa na Serikali wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze leo Jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa vyombo vya Habari nchini kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya viwanda. Wanaomsikiliza kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na . Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas
Mkurugenzi wa Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akichangia wakati wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo vya Habari ikiwa ni muenedelezo wa vipindi vya Wadau Tuzungumze kinachoratibiwa na Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lengo likiwa ni kuimarisha ushirikaiano baina ya Wizara na wadau wa sekta zake.
PICHA NA MICHUZI JR.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni