MBUNGE
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi madawti kwa viongozi
wa kata ya sao hill kwa ajili ya matumizi ya shule
MBUNGE
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipongezwa na viongozi wa kata
ya sao hill kwa jitihada wanazozifanya kuleta maendeleo katika jimbo la
mafinga mjini
Chumi
alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifungo 10 ya
saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na KinyanamboNa Fredy Mgunda,Mafinga.
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ameendelea kutatua changamoto mbalimbali za jimbo hilo kwa kufanya ziara kwenye baadhi ya shuleza msingi zilizopo katika mjini wa mafinga na kukagua baadhi ya miundombinu inayoendelea kukarabatiwa kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
Katika ziara hiyo Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifuko 10 ya saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo ambayo yalitolewa na wakala wa shamba la miti Sao Hill huku chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mafinga Mji kupitia mwenyekiti wake Yohanes Cosmas wakichangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mbunge za kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni