Mkuu
wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth
Nzuki akiwasilisha malengo ya warsha kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida kufungua warsha hiyo.
Wajasiriamali
kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kupata
nafasi ya mafunzo yanayohusu fursa mpya zinazopatikana katika kilimo cha
biashara katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF).
Elimu
ambayo wajasiriamali waliipata katika warsha hiyo ni elimu ya shamba
kitalu na ujasiriamali, elimu ya kilimo cha foda na mbogamboga, elimu ya
kilimo na kufuga samaki katika matanki, elimu ya ufugaji samaki katika
mabwawa, elimu ya ufugaji samaki katika vizimba, kutazama fursa zilizopo
katika ufugaji bora wa kuku na kupata elimu kuhusu Azolla ambayo
inaweza kutumika kama chakula cha mifugo na pia kama mbolea.
Akizungumza
katika warsha hiyo mmoja wa wawasilishaji mada, Dominic Haule alisema
kilimo kina fursa nyingi lakini watu wengi wanashindwa kufanikiwa
kutokana na kuwepo mambo mbalimbali ambayo yanayakwamisha.
Alisema
changamoto hizo ni pamoja na kukosa elimu ya kilimo na kushindwa kupata
taarifa sahihi za kiteknolojia kuhusu kilimo cha kisasa.
“Tunahitaji
kutazama fursa zilizopo, zipo nyingi lakini bado tunakabiliwa na
changamoto wakulima wanakosa elimu ya kilimo kujua hata mazao bora
yanakuwaje, bado kuna shida ya pembejeo na mitaji inakuwa changamoto
maana ili ufanikiwe unahitaji uwekezaji mkubwa,” alisema Haule.
Awali
akitoa neno la ufunguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida alisema Tanzania ina maeneo
mazuri ya kufanyia kilimo na kinachohitajika ni wakulima kutambua njia
za kufanya kilimo bora ili watakapoanza kulima waweze kupata matokeo
mazuri kwa aina ya kilimo wanachofanya.
“Uchumi
wa nchi unategemea kilimo, nchi yetu ina eneo zuri la kilimo lakini
bado kuna changamoto kama mabadiliko ya hali ya nchi ni vyema kukutana
na kujua njia bora za kutumia kabla ya kuanza kufanya kilimo,” alisema
Dkt. Kida.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akifungua warsha ya siku moja yenye lengo la kutambulisha na
kuelimisha zaidi wananchi kuhusu fursa mpya za kibiashara ambazo
zinapatikana katika sekta ya Kilimo.
Mshereheshaji katika warsha ya kutazama fursa mpya katika kilimo biashara, Abdallah Hassan.
Mwakilishi
wa Wizara ya Kilimo, Mifungo na Uvuvi , John Mapunda akielezea nafasi
ya serikali kuwasaidia wajasiriamali ili kufikia malengo yao katika
warsha ya siku moja iliyoandaliwa na ESRF.
Pichani
juu na chini ni umati wa washiriki kutoka mikoani na maeneo mbalimbali
ya jiji la Dar es Salaam waliohudhuria warsha hiyo iliyoandaliwa na
ESRF.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akifurahi jambo na mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Mifungo na
Uvuvi, John Mapunda katika warsha hiyo.
Dominic Haule kutoka chuo cha iMADS akielezea kuhusu shamba kitalu na ujasiriamali.
Bw.
Abdullatif Mbulo kutoka Horti Ogranics Ltd, akielezea kuhusu kilimocha
foda na mbogamboga, sambamba na ufugaji wa samaki katika matanki.
Luteni
Joseph Lyakulwa, kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akizungumzia
Ufugaji wa Samaki katika Vizimba katika warsha hiyo iliyohudhuriwa na
wajasiliamali mbalimbali.
Pichani
juu na chini washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Kilimo Biashara.
Pichani
juu na chini washiriki wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada katika
warsha ya siku moja ya Kilimo Biashara iliyoandaliwa na ESRF.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni