KITUO CHA POLISI CHASHAMBULIWA


Wapiganaji wa kundi la waasi wa FDLR washambulia kituo cha polisi nchini Rwanda.

Jeshi la Rwanda limethibitisha kuwa kituo kimoja cha polisi cha eneo la Bugeshi, Kaskazini Magharibi kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimeshambuliwa na wapiganaji wa kundi la FDLR.

Kulingana na naibu msemaji wa jeshi la Rwanda Luteni kanali Rene Ngendahimana,wapiganaji wanaokadiriwa kuwa kati ya 20 na 30 wa FDLR wamevuka eneo hilo la mpakani mnamo usiku wa manane kuamkia leo na kushambulia kituo hicho cha polisi.

Wapiganaji wa kundi la waasi wa FDLR washambulia kituo cha polisi nchini Rwanda. 

Hata hivyo hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu idadi ya waliokufa au kujeruhiwa katika shambulio hilo, ila katika tanganzo linalopatikana kwenye ukurasa wa twitter wa jeshi la Rwanda, naibu msemaji wa jeshi amesema kuwa jeshi la Rwanda linadhibiti eneo hilo na kwamba taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo zitatolewa baadaye.

Mwezi uliopita, eneo hilo pia lilishambuliwa na wapiganaji waliotajwa kuwa wa kundi la FDLR ambapo taarifa ya jeshi la Rwanda ilisema kuwa mpiganaji mmoja wa FDLR aliuawa.BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni