Afisa wa Vijana wa Muungano wa Siasa
wa ODM, amepigwa risasi jana usiku na kufa akiwa nje ya geti la
nyumba yake eneo la Ruai, Jijini Nairobi.
Afisa huyo Stephen Odongo Mukabana,
42, alishambuliwa wakati akingojea kufunguliwa geti, kwa mujibu wa
Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Ruai, Kayole OCPD Ali Nuno.
Mukabana alivamiwa na watu sita,
ambapo mmoja wao alikuwa na bastola ambayo alitumia kumpiga risasi
kichwani na tumboni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni