CRISTIANO RONALDO ACHARUKA NA KUIBEBA REAL MADRID NUSU FAINALI UEFA

Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu mazuri wakati Real Madrid ikibadili matokeo ya mchezo wa awali waliofungwa mabao 2-0 na Wolfsburg na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wolfsburg waliwasili Hispania wakiwa na nia ya kulinda ushindi wao wa nyumbani, lakini walijikuta mipango yao ikitibuliwa na Cristiano Ronaldo ndani ya dakika 77 tu kwa kucheka na nyavu mara tatu na kufanya matokeo kuwa 3-0.
                                                    Cristiano Ronaldo akipachika goli la kwanza 
                  Cristiano Ronaldo akiruka juu na kupachika goli la pili kwa mpira wa kichwa
Katika mchezo mwingine Manchester City wametinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya Kevin de Bruyne kufunga goli latika dakika za mwisho na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Paris St-Germain.

Baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wao wa kwanza Jijini Paris na mchezo huo kubakiwa ukitegemea matokeo yoyote baina ya timu hizo mbili, huku Sergio Aguero akijikuta akikosa penati katika nusu ya kwanza ya mchezo huo wa jana.
                 Kevin de Bruyne akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika bao pekee

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni