Na Neema Mwangomo
Waumini
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima
jana wamejitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
wagonjwa
wanaohitaji damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Katika
shughuli hiyo ya utoaji damu MNH kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa
Damu Salama, Kanda ya Mashariki wamefanikiwa kukusanya chupa nyingi za
damu.
Akizungumzia
shughuli hiyo Ofisa Uhamasishaji wa Damu salama wa MNH, Hamisi Kubiga
amesema kwamba mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa kwani
kwa siku chupa zinazotakiwa kukusanywa ni 70 hadi 100 ili kuweza kukidhi
mahitaji ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Kubiga
amesema kuwa baadhi ya makundi ambayo yanauhitaji mkubwa wa damu ni
kina mama wajawazito, majeruhi, na wagonjwa wa saratani hivyo amewaomba
Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
wagonjwa.
“Hivi
sasa tunaendesha mpango wa uchangiaji damu, tunashukuru wapo wananchi
wamejitokeza lakini bado tunawaomba wananchi, taasisi kampuni binafsi na
umma waje kwa wingi ili kwa pamoja tuwasaidie wenzetu wenye uhitaji,”
amesema Kubiga.
Shughuli ya utoaji damu inaendelea jumapili ijayo kwenye kanisa hilo la Ufufu na Uzima.
Endapo
taasisi, kanisa, shule na makundi mengine yanataka kuchangia damu.
Wawasiliane na Mkuu wa Idara ya Maabara wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kwa namba 0754 575 981, Mkuu wa Idara ya Maabara namba0713 777 595 na Ofisa Uhamasishaji wa Damu salama wa hospitali hiyo namba 0754 597 165.
Waumini
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaongozwa na Askofu Josephat Gwajima
wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
wagonjwa wenye mahitaji ya damu. Shughuli hiyo imefanywa na
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa
wa Damu Salama. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
Mshauri
wa MN, Erica Ishengoma akiandika maelezo baada ya kumsikiliza mmoja wa
waumini wa kanisa hilo, huku wengine wakiwa kwenye foleni kabla ya kutoa
damu.
Ofisa
Uhamasishaji wa uchangiaji damu salama, Hamisi Kubiga (kulia) na Erica
Ishengoma wakiwapatia chupa maalumu za kuweka damu baada ya kupima
uzito.
Damu ikitolewa
Mtaalamu wa maabara Anthony wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akiendelea na shughuli ya utoaji damu katika kanisa hilo.
Wataalamu
wa maabara, Peter Onesmo (kulia) na Anthony (wa pili kulia) wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiendelea kutoa damu baada ya
waumini hao kujitokeza kwa wingi katika kanisa hilo lilipo Ubungo
jijini Dar es Salaama.
Muumini wa kanisa hilo, Vedasto Aloysi akitolewa damu katika kanisa hilo na mtaalamu wa maabaram Peter Onesmo.
Damu iliyotolewa na waumini wa kanisa hilo
Hawa
Hamisi (18) akichangia damu . Hawa amesema kuwa anasikia fahari
kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu katika
hospitali hiyo.
Waumini wa Askofu Gwajima Watia Fora Utoaji Damu Muhimbili
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea kujitolea kutoa damu leo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea kutoa damu Ubungo jijini Dar es Salaam.
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea kutoa damu Ubungo jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni