Makamu
 wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi wa 
wanaosafiri mara kwa mara  kwa ajili ya harakati zao za maisha kuchukua 
vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili kujikinga na maradhi ya 
Malaria.
Akizungumza
 katika Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya 
Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema licha ya Zanzibar kuwa na 
kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria, utafiti unaonyesha watu 
wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni wale wenye utaratibu wa 
kusafiri nje ya Zanzibar.
Amesema
 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa dhati kuimarisha afya
 za wananchi na itaendelea kuboresha huduma za afya sehemu zote na 
kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
Hata 
hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia mafanikio katika vita dhidi ya 
Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea kuwa tishio  kwa 
wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa 
afya.
Mapema
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik Akili alisema katika kumaliza 
Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa vyandarua  760,000 
vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote za Zanzibar.
Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.
Katika
 maadhimisho hayo, wananchi na vikundi vya mazoezi wakiongozwa na Makamu
 wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari yaliyoanza Mazizini, 
Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar.
Makamu
 wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (katikati) akiongoza 
Matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo 
yamefanyika kuanzia mazizini na kumalizikia maisara mjini Unguja.kulia 
yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kushoto yake ni 
katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt  Juma Malik Akili.
Vikundi
 vya mazoezi vikiwa katika matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya 
Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia Mazizini Wilaya ya Magharibi B
 na kumalizikia Maisara Mjini Unguja.
Vikundi
 mbalimbali vya Mazoezi vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika 
Uwanja wa Maisara katika maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo 
yamefanyika  Mjini Unguja.
Waziri
 wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (wa mwanzo ) akishiriki katika mchezo wa 
kuvuta  kamba kwenye maadhimisho hayo ambapo timu ya Baraza la 
Wawakilishi ilipambana na Wizara ya Afya ambapo  Afya ilipata ushindi. 
Waziri
 wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi katika 
Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika viwanja vya 
Maisara Mjini Unguja.
Makamu
 wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya 
Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika Maisara Mjini 
Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na 
Kushoto yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni