Wananchi
wa kijiji cha Malekichanda kilichopo katika kata ya Mang’ola wilayani
karatu mkoani Arusha wamelalamikia kitendo cha serekali kufungia ziwa
Eyasi na kusema kuwa kitendo hicho kimewafanya vijana wengi kukosa kazi
na kinaweza kusababisha wananchi wa eneo hilo kukumbwa na baa la njaa
kutokana na kumaliza chakula chote ambacho walikuwa wamekihifadhii kwa
ajili ya chakula cha akiba akiba.
Hayo waliyasema leo wakati Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka
Hamdu Shaka alipofanya ziara yakutembela na kukagua baadhi ya miradi
inayofanywa na chama pamoja na kuongea na wananchi wa kata hiyo.
Walisema
kuwa wanasikitishwa sana na kitendo cha mkuu wa
wawilaya kuwasimamisha shughuli zao za uvuvi kwani ndizo walizokuwa
wakizitegemea katika kujipatia kipato pamoja na chakula katika kijiji
hicho na kata kwa ujumla.
Mmoja
wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Kristopher Nyato alisema
kuwa tangu marchi 19 walizuiwakufanya shughuli zao za uvuvi katika eneo
hilo na kupewa masaa 24 kuondoka katika eneo hilo kwakile kilichodaiwa
kuwa eneo hilo limekubwa na ugonjwa wa kipindu pindu.
“unajua mimi ni
mfanya biashara nimetokea mbali nasio mimi tu tupo wengi naninavijana
wangu ambao nimekuja nao hapa kwa ajili ya shughuli hii ya uvuvi
sasa tarehe hiyo 19 mwezi wa tatu mkuu wawilaya alikuja apa na askari
nakutupa masaa 24 tuwe tumeondoka kuhoji nini ni wakatuambia ni
pachafu mara waseme kuna kipindu pindu tukawaambia kama ni pachafu
watuache wakagoma wakasema tumesema muondoke ndiposisi kwa kuwa
tunaogopa nakamaunavyojua wananchi tulivyo waoga tukaondoka na
tulivyoondoka walituambia baada ya siku chache wangefungua lakini adi
sasa apajafunguliwa tunateseka sana ata vyakula vyetu vya akiba
tumemaliza yaani apa ni tabu tu”alisema Nyato
Kwa
upande wa mwananchi mwingine aliejitambulisha kwa jina la Wiliam Jonas
alisema kuwa mara baada ya ziwa hilo kufungwa wamekuwa wanaishi maisha
ya kuomba omba ,wao kama wananchi wanagawana chakula walichokuwa
wamekiifadhi na kinakaribia kwisha na vijana wengi walikuwa wakifanya
shughuli za uvuvi katika ziwa hilo wamekuwa wazururaji.
Akiongea na wananchi hao Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka
Hamdu Shaka alisema kuwa yeye kama katibu amesikia malalamiko yao
naatayafanyia kazi kwa kukutana na mkuu wawilaya nakuona ni jinsi gani
ambavyo wataweza kutatua tatizo hilo.
Gazeti hili halikuishia hapo ilibidi kumtafuta mkuu wa wilaya ya karatu Omary Kwaanq
ili kuzungumzia tuhuma hizi nakusema kuwa kweli wamelifunga ziwa hilo
kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu ambao umeikumba wilaya yake .
Alisema
kuwa mpaka sasa wilaya yake ina wagonjwa 70 wa kipindu pindu na
wamefanya utafiti ukaonyesha wagonjwa wengi wametokea maeneo ya ziwa
hilo.
“tumefanya
utafiti kiukweli kwa kushirikina na mtaalamu wamagonjwa wa milipuko
nakubaini kuwa maji yale ya ziwa yana chembe chembe za wadudu wanao
eneza ugonjwa wa kipindu pindu hivyo tukaamua ni borakufunga ziwa ilo
ili wananchi wasiendelee kuzurika na ugonjwa huo.
Aliongeza
kuwa mara baada ya kuona maji yale ya ule mto yana vimelea vya ugonjwa
wa kipindu pindu ndio maana wakaona ni bora wafunge ziwalile ili
wananchi wasiendele kupata ugonjwa huo hatari.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa
anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hiii leo wakati alipofanya
ziara katika kata hiyo iliopo ndani ya wilaya ya karatu mkoani Arusha
Diwani
wakata ya mang'ola Lazaro Gege akiwa anampa maelezo kwa ufupi ya
mradi wa matofali kaimu katibu mkuu wa vijana CCM taifa
Mwenyekiti
wa umoja wa vijana wa ccm Mkoa Arusha Sabaya Lengai akiwa anaongea na
wananchi wa kata ya Mang'ola hii leo wakati wa ziara ya kaimu katibu
mkuu wa vijana taifa
|
baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kufatilia mkutano huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni