Balozi
wa Kimataifa wa UNAIDS, Mette-Marit akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kazi anazofanya kama balozi wa UNAIDS kwa kipindi cha miaka 10
tangu aanze kazi hiyo. (Picha na Rabi Hume wa Modewjiblog)
Katika
kuhakikisha watu wanaoishi na UKIMWI wanaishi kwa furaha bila
kunyanyapaliwa na watu wanaowazunguka, jamii imetakiwa kuwa na mtazamo
tofauti kwa watu wanaoishi na ugonjwa huo.
Hayo
yalisemwa na mke wa mtoto wa mfalme wa Norway, Mette-Marit ambaye pia
ni balozi kimataifa wa Shirika la Umoja la kupambana na HIV na UKIMWI
(UNAIDS) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi
anazozifanya kwa UNAIDS kama balozi ambaye anazunguka maeneo mbalimbali
duniani ili kuelimisha jamii kuhusu UKIMWI.
Mette-Marrit
alisema kuwa watu wenye UKIMWI ni kama watu wengine hivyo wana haki ya
kupata huduma bila kunyanyapaliwa ili waweze kuishi kwa uhuru kama watu
wengine na ili kufanikisha hilo ni wajibu wa kila mtu kuwasaidia
waathirika.
“Watu
kuwa na UKIMWI sio mwisho wa maisha inatakiwa kwanza jami kuwa na
mtazamo tofauti na inatakiwa kila mtu kusaidia mapambano ya UKIMWI sio
jambo la mtu mmoja mmoja,” alisema Mette-Marit.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho
akizungumzia kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambano ya
UKIMWI.
Nae
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatma
Mrisho alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili
kupambana na UKIMWI lakini pia ili kufanikisha mapambano hayo wanahitaji
kushirikiana na taasisi ambazo zitawasaidia katika mapambano hayo.
Lakini
pia Dkt. Mrisho amezitaka serikali za mitaa kuacha kusubiri mpaka
serikali imepeleke pesa ndiyo wawasaidie watu wanaoishi na UKIMWI na
hivyo waweke utaratibu wa kutumia sehemu ya mapato yao ili kusaidia
mapambano hayo.
“Serikali
haijalala katika mapambano tunahitaji kushirikiana na taasisi ambazo
zinatusaidia kupunguza maambukizi mapya na tunaona Mette-Marit amekuwa
akifanya jambo zuri anazunguka sehemu nyingi ili kusaidia kupunguza
maamukizi mapya ya UKIMWI,” alisema Dkt. Mrisho.
Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi, UNAIDS nchini Tanzania, Warren Naamara akizungumzia ugonjwa wa UKIMWI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni