WATU 25 WAUWAWA NA MAKUMI KUJERUHIWA KATIKA MASHAMBULIZI IRAK

Watu wapatao 25 wameuwawa na makumi kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu kwenye maeneo mbalimbali ya Irak.

Walipuaji wapatao 10 wamefanya mashambulizi hayo, ambayo yameelezwa yalikuwa yanawalenga maafisa wa vikosi vya usalama na washirika wao wa kikundi cha Shia.

Kundi la Dola ya Kiislam (IS) ambalo linashikilia eneo la kaskazini na mashariki limesema limehusika na mashambulizi hayo.

Katika moja ya shambulio baya mtu aliyejitoa mhanga alijilipua na kuuwa watu 14 kwenye hoteli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni