Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akijiandaa kuzungumza na
Wanafunzi na wanachama wa CCM waishio Mji wa Beijing nchini China.
Rais
Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na wanafunzi na Wanachama wa
CCM, waishio nchini China, wakati alipokutana nao akiwa katika ziara
yake nchini humo.
**************************************
Na Mwandishi Wetu, Beijing China
Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe
20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la
Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika
Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State
Guesthouse jijini Beijin, nchini China.
Wakisoma
risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na
miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt.
Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kwamba wako
tayari kurudi nyumbani na kutumia elimu zao katika kuhakikisha kuwa
maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa.
Katika
mazungumzo na Wanachama hao, Mhe Kikwete amewakumbusha jukumu kubwa
lililo mbele yao la kujenga Chama na kulijenga Taifa la Tanzania, katika
hotuba yake ameeleza kuwa China imefanya Mapinduzi makubwa katika
maendeleo na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hiyo, hivyo kuwataka
kujifunza na kuchukua maarifa ya China na kuyatumia wakirudi nchini ili
kufanikisha Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.
Mheshimiwa
Kikwete na Ujumbe wake wanatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou hapo
kesho na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa
CCP na Rais wa Serikali ya watu wa China Mhe Xi Jinping, pamoja na
kufanya mazungumzo muhimu na Viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China
{CCP} katika jimbo hilo.
Rais
Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na wanafunzi na Wanachama wa
CCM, waishio nchini China, wakati alipokutana nao akiwa katika ziara
yake nchini humo.
Picha ya pamoja baada ya mazungumzo yake na wanaccm na wanafunzi wwatanzania waishio China.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni