MAPIGANO MAKALI YATOKEA KATIKA JIJI LA BRAZZAVILLE

Mapigano ya silaha nzito yamesikika katika barabara za Brazzaville mji mkuu wa Jamhuri ya Congo ambapo vikosi vya usalama vimepelekwa.

Kituo kimoja cha polisi na jengo moja la serikali lilishambuliwa Jumatatu asubuhi kwenye wilaya ya Makelekele.

Serikali ya Jamhuri ya Congo imelishutumu kundi linalojiita Ninja kwa kufanya mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo yamefanyika ikiwa ni wiki chache kupita baada ya rais Denis Sassou Nguesso kushinda urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi uliotiliwa shaka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni