TAARIFA KWA NYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam – 11 April 2016 –fastjet,
 shirika la  ndege la gharama nafuu barani Afrika imeshinda Tuzo ya 
Shirika la Ndege Linaloongoza Afrika kwa Gharama Nafuu kwenye Tuzo 
ya  23 ya Mwaka  ya  Usafiri Duniani iliyotolewa Zanzibar, 
Tanzania  Aprili 9, 2016.
Tuzo
 ya Usafiri ambayo inatambulika  duniani  imepangwa kwa kutambua, 
kutuza na kusherehekea  mafanikio kwenye  sekta zote muhimu  za 
usafirishaji  wa kwenye sekta ya utalii.
 Tuzo
 ya Shirika la Ndege Linaloongoza kwa Gharama Nafuu  ambayo hutolewa kwa
 wataalamu wa  usafiri na utalii pamoja an watumiaji duniani 
kote  inatokana na kutambua  huduma za fastjet za kufanya watu wamuumudu
 usafiri wa anga, usalama na kuaminika  kwenye mtandao yote barani 
Afrika.
“Kutambuliwa
 na kupata tuzo hii sio tu kunaonesha  kujituma kwa ufanisi kwenye 
usafiri wa anga, lakini kunaonesha matokeo ya juhudi zetu  tunazojaribu 
kulifanyia bara la Afrika,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet 
Tanzania,  John Corse na kuongeza, “tunajivunia sana  kupokea 
kutambuliwa huko na sekta hii kubwa  na fastjet itaendelea  kuufanya 
usafiri wa anga  kuwa wa gharama za chini ambazo watu wengi 
watazimudu  barani Afrika.”
Shirika
 hilo la ndege la bei nafuu  lilizinduliwa  Novemba 2012 na linafanya 
safari kadhaa za ndani ya Tanzania  kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya, 
Mwanza na Kilimanjaro. Kukua kwa mtandao wa fastjet  pia kunatoa 
huduma  kwa njia ya kutoka Dar es Salaam na Zanzibar na kwenye vituo vya
 kimataifa  kama vile Johannesburg, Harare, Victoria falls, Entebbe, 
Nairobi na Lusaka.
Fastjet
 inatarajia  abiria wake wengi kwenye njia hizo inakotoa huduma  kuwa 
ndio wanasafiri kwa mara ya kwanza kwa kutumia ndege  kutokana na sababu
 ya kukwazwa na tozo za nauli ya juu  ambazo awali  hawakumudu kulipa 
kwa ajili ya usafiri huo.
Huduma
 hii ya nauli nafuu imeungwa mkono kwenye utafiti uliofanywa na shirika 
hilo hivi karibuni, unaoonesha kuwa asilimia 40 ya abiria  kwenye njia 
zote walikuwa ndio mara yao ya kwanza kusafiri kiumudu kusafiri kwa 
ndege  kwa mara ya kwanza  hivyo pongezi ziende kwa gharama nafuu za 
fastjet.
Jambo
 jingine ambalo linapatikana kwenye  njia inamopita fastjet ni 
kuboreshwa kwa mbadala wa mzigo  ambako kunajulikana kama ‘freighty’ 
kunakoruhusu abiria  kusafirisha  hadi kilo 80 zilizofungwa kwenye 
mabegi kwa  gharama ya shillingi 88,000. Mbadala huo wa kusafirisha 
mizigo kimsingi umekuwa ni maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na 
fastjet  kwenda kununua bidhaa za jumla kimataifa na kuzisafirisha kwa 
ajili ya kuziuza  kwenye masoko ya  nyumbani mwao.
 Tuzo
 hii inaongeza  idadi ya tuzo  ambazo fastjet 
imeshazipata  zikiwemo kushinda Tuzo ya Ubunifu kwenye Usafiri kwenye 
utoaji wa nane wa tuzo hiyo mwaka 2015, na hali kadhalika  kutangazwa 
kuwa  shirika la ghama  nafuu barani Afrika katika 
kulinganishwa  mengine kwenye usafiri wa anga kupitia mtandao wa 
safiri  WhichAirline.com in 2016.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni