Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema ambaye alikuwa mgeni rasmi wa
uzinduzi wa Michuano ya Shule za Sekondari Nchini (UMESETA), akipiga
dana dana wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es
Salaam leo.
Wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto), akikabidhi vifaa vya
michezo kwa Shule ya Sekondari ya Azania vilivyotolewa na Kampuni ya
Coca Cola. Kulia Ofisa kutoka kampuni ya Coca Cola wadhamini wakubwa wa
michuano hiyo kwa mwaka 2016.
DC
Mjema akisalimiana na mwamuzi wa mchezo kati ya timu ya Sekondari ya
Tirav ya Yombo na Makongo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es
Salaam. Makongo ilishinda mabao 2-1.
DC Mjema akiwasalimia wachezaji wa timu ya Tirav.
DC Mjema akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari.
Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema (kulia), akitoa nasaha zake kwa wachezaji hao kabla ya kuanza kucheza.
DC Mjema hapa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya sekondari ya Tirav na viongozi mbalimbali.
DC Mjema hapa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya sekondari ya Makongo na viongozi mbalimbali.
Hapa akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo huo na viongozi mbalimbali.
Hapa mtanange ukiendelea.
Golikipa wa timu ya Tirav, Abdul Badi akiokoa moja ya hatari katika lango lake.
Wachezaji wa timu ya Makongo wakishangilia baada ya kupata bao lao la kwanza.
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema amezindua michuano ya Shule za
Sekondari Nchini (UMESETA) katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
huku akisisitiza kuwa yataendelea kuwaibua wachezaji wengi chipukizi.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mjema aliishukuru kampuni ya Cocacola kwa kudhamini
mashindano hayo huku akiyaomba makampuni na wadau wengine kujitokeza
kudhamini michezo mbalimbali.
Mashindano
hayo yatashirikisha timu zaidi ya 40 katika mchezo wa mpira wa kikapu
kwa vijana wa Shule za Sekondari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini
huku ikishirikiana na waandaaji wa michuano ya michezo ya Shule za
Sekondari UMISETA katika kuhakikisha wanapata wachezaji wenye elimu
kutoka mikoa yote hapa nchini.
Akizungumzia
mashindano hayo Meneja wa Biashara wa Coca Cola Maurice Njowoka
alisema wameamua kuongeza mchezo ili kupanua wigo wa mashindano hayo
hapa nchini.
Aidha
alisema lengo la kuungana na waandaaji hao, badala ya Shirikisho la
soka Tanzania (TFF) pekee ni kutaka kupata wachezaji sahihi, kutoka
mikoa yote, na ambao wako katika mashule ya Sekondari.
"Hii itatusaidia kupata wachezaji sahihi wenye elimu na ambao kweli wanasoma shule za sekondari,"alisema Njowoka.
Alisema tofauti na mwaka jana, tuliwatumia TFF pekee jambo ambalo tulipata wachezaji lakini katika mazingira magumu zaidi.
Alisema
michuano ya mwaka huu wanaimani watapata wachezaji kiurahisi kwa sababu
UMISETA ina rekodi ya wanafuzni wanaosoma katika shule za sekondari.
Njowoka
alisema kwa kuanzia jijini Dar es Salaam, wametoa jezi na vifaa kwa
shule za Sekondari zilizohudhuria katika mashindano hayo.
Alisema
baada ya Dar es Salaam, wanaelekea Mwanza, Mbeya, Arusha na Moshi kwa
ajili ya kuzindua rasmi michezo hiyo ambayo shule zinaanza kufanya
mazoezi kwa ajili ya kujiandaa.
Alisema
katika udhamini wao watatumia kinywaji cha Coca Cola kwa upande wa
soka, wakati Kikapu watatumia Sprite, lengo ni kufanikisha michuano hiyo
safari hii kutokana na kuongeza idadi ya mchezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni