POLISI 47 WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA MAUAJI YA MASINGASINGA

Maafisa polisi 47 wamehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama maalum ya India baada ya kupatikana na hatia ya kuwauwa Mahujaji Masingasinga 10 mnamo mwaka 1991 na kisha kudanganya ili kujaribu kuhalalisha kitendo hicho.

Maafisa 10 wa polisi waliokuwa wakishtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji ya kutumia silaha, walishakuwa wamekufa kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo.

Maafisa polisi hao walitiwa hatiani kwa kupanga mauaji ya watu kwa kuandaa jaribio feki la kukabiliana na wahalifu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni