Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa wanahabari,
mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka Jijini
Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini Kampala. Mbali
na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi
nyingine za Afrika Mashariki na Kati.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia),
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo
(wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James
Mataragio walipokuwa wakimsubiria Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo alierejea jijini Dar es salaam leo akitokea Jijini
Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi
Tanga.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni