Habari na picha na John Nditi, Morogoro
WAZAZI na walezi wenye watoto wenye ulemavu wilayani Mvomero , mkoa wa Morogoro wametakiwa kuwapeleka shule ili waweze kupata elimu itakayokuwa ni mkombozi wao kwa maisha yao ya baadaye katika kujiletea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi, imeelezwa.
Rai
hiyo ilitolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, George
Jackson Mbijima ,Aprili 20, 2016 wakati wa uzinduzi wa Darasa la watoto
wenye ulemavu , katika kijiji cha Changarawe, Kata ya Mzumbe , wilayani
humo.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru , Mbijima , alitumia fursa hiyo kuwataka
wazazi na jamii kwa ujumla, kuwapeleka watoto wenye ulemavu katika shule
hiyo kwa kuwa elimu pekee ndiyo itakayowakomboa.
“
Serikali ya Tanzania imeweka mazingira mazuri ya kusoma kwa watoto wa
makundi yote wakiwemo wenye ulemavu wa aina mbalimbali , kwani elimu
pekee ndiyo mkombozi wao katika suala la kujitegemea siku za
usoni...hivyo jamii itambua hilo na kuwajali watoto wenye ulemavu na si
kuwaficha majumbani” alisema Mbijima.
Naye
Mwalimu wa darasa la watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi ya
Changarawe , Doreen Msuya, aliiomba serikali ya Wilaya, mkoa na
Serikali kuu, kuona uwezekano wa kujenga hosteli ya watoto wenye ulemavu
katika eneo la shule hiyo.
Msuya
alisema , hatua hiyo itawezesha watoto wengi wanaoshindwa kufika
kutokana na ulemavu wao waweze kuishi karibu na shule na kunufaika na
elimu ambayo itawasaidia katika maisha yao baadae.
Hivyo
alisema , mradi huo wa darasa la wanafunzi wenye mahitaji maalumu
ulianzishwa mwaka 2013 baada ya kufanyika sense ya watoto wenye mahitaji
maalumu na kubaini watoto 26 ambao kwa kipindi hicho walikauwa
majumbani ingawa umri wa kuanza shule ulikuwa umefika.
Msuya
alisema , mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana kati ya halmashauri
ya wilaya ya Mvomero na wanajamii wa kijiji cha Changarawe ambao hadi
sasa wanafunzi 42 wapo darasani , kati ya hao wavulana 27 na wasichana
15.
“
Kupitia mradi wa darasa hili umeweza kuibua watoto sita waliokuwa
wamefichwa nyumbani ambao ni wenye ulemavu wa aina mbalimbali” alisema
Msuya.
“
Kuazishwa kwa darasa la watoto wenye ulemavu katika shule hii ya
Changarawe kumesaidia kuibuliwa ndani ya jamii watoto wa aina hiyo
waliokuwa mitaani na nyumbani bila ya matumaini yeyote ya baadaye “
alisisitiza Mwalimu Msuya.
Akisoma
risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake , mwanafunzi wenye ulemavu ,
Steven Petro (14) wa darasa la tano shuleni hapo, kuanzishwa kwa darasa
hilo kumewawezewa wao kupata elimu na hivyo kuwa na matarajio mazuri ya
siku za usoni.
Naye
mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa, alihimiza wazazi kuhakikisha
watoto wanapata fursa ya kuandikishwa shule ya awali na msingi ikiwa na
kuwandeleza hadi elimu ya juu kwa vile elimu ndiyo ufunguo wa maisha.
Mwenge
wa Uhuru ukiwa katika wilaya ya Mvomero ulipitia, kuzindua, kuweka
mawe ya msingi na kuonwa miradi mitano ya maendeleo yenye thamani
zaidi ya Sh milioni 688.6 ukiwemo wa darasa la watoto wenye mahitaji
maalumu.
Tayari
Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake katika Manispaa ya Morogoro,
halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Mvomero , Ulanga na Kilombero tangu
ulipozinduliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan , Aprili 18, mwaka
huu katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.
Baadhi
ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga , mkoa wa Morogoro
wakifuatilia jambo wakati wa ugeni wa Mwenge wa Uhuru .
Kikundi cha Wanawake cha Mvomero kikionesha bidhaa zao.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa , George Jackson Mbijima akifuatana
na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Betty Mkwasa kuangalia
bidhaa za kikundi cha wanawawake.
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, George Jackson Mbijima akimkabidhi
hati kwa klabu ya wapinga rushwa ya Twikale wose Lugono, Mwenyekiti wa
klabu , Kondo Mahawa.
Mgangazaji
wa TBC Swedi Mwinyi , ( kati kati ) akiwa pamoja na mshereheshaji
mwenzake ( kushoto) wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2016,
uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.
Mjasilimali
wa Kimasai akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
pamoja na mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa.
Mkuu
wa Takukuru wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Eufrasia Kayombo (
kushoto) akisaini hati ya uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa Twikale
wose , Lugono kilichopo wilaya ya Mvomero.
Mkuu
wa wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Betty Mkwasa akiwa ameushika
Mwenge wa Uhuru , baaada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,
Muhingo Rweyemamu ( hayupo pichani).
Mkuu
wa wilaya ya Ulanga, mkoa wa Morogoro, Christina Mndeme, ( kulia)
akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe (
kushoto),kuanza mbio zake Aprili 22, 2016
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa , wakitoka kuweka jiwe la msingi jengo la kuhifadhia dawa na vifaa tiba katika hospitali ya wilaya ya Ulanga. |
Mmoja
wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru,
baada ya kuvuka katika kivuko cha Mv Kilombero 11 kutokea wilaya ya
Ulanga. (1)
Mwanafunzi
mwenye ulemavu wa viungo, Steven Petro wa darasa la tano shule ya
Msingi Changarawe, wilaya ya Mvomero akisoma risala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni