BALOZI SEIF AKUTANA NA MASHEHA WA WILAYA ZA MAGHARIBI A NA B

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Masheha wa Wilaya za Magharibi “A “na “ B” pamoja na wakuu wao wa Wilaya na Mkoa hapo katika Ukumbi wa Kikosi cha Valantia {KVZ} Mtoni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi wa kwanza kutoka Kushoto akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Ndugu Mwinyiusi Khamis na yule ya Magharibi “B”Nd. Ayoud Mohammed Mahmoud wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akizungumza na masheha wa wilaya zao.
Baadhi ya Masheha wa Wilaya za Magharibi A na B wakisikiliza hotuba ya Balozi Seif wakati alipobadilishana nao mawazo kuhusu suala la migogoro ya ardhi katika maeneo yao
Baadhi ya Masheha wa Wilaya za Magharibi A na B wakisikiliza hotuba ya Balozi Seif wakati alipobadilishana nao mawazo kuhusu suala la migogoro ya ardhi katika maeneo yao
Balozi Seif akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Masheha wa Wilaya za Magharibi A na B hapo Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia Mtoni.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum ya SMZ Mh. Haji Omar Kheir na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum ya SMZ Mh. Haji Omar Kheir akitoa msimamo wa Wizara yake katika kutekeleza agizo la Rais wa Zanzibar kuhusu migogoro ya ardhi.

Kushoto ya Mhe. Haji Omar ni Makamu wa P;ili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Kulia ya Mh. Haji ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na Naibu wake Mh. Juma Makungu Juma.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Bwana Moh’d Omar Said akichangia mawazo katika mkutano wao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia {KVZ} Mtoni. Picha na - OMPR – ZNZ.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni