Timu
 ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania Bunge 
Sports Club inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo mkali na wa aina 
yake ambao ni wa kwanza na timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya 
Mapinduzi Zanzibar.
Mapema
 leo Aprili 25.2016 timu hiyo ilishuka katika dimba hilo la Amani na 
kupasha misuli maalum kwa hiyo mchezo huo wa hiyo kesho ambapo kwa 
mujibu wa viongozi wa timu hiyo ya Bunge wametamba kuibuka na ushindi wa
 kishindo.
Kocha
 wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. 
Venance Mwamotto ametamba kwa timu yake kuibuka na ushindi mnono katika 
mchezo huo kwani wana mazoezi ya kutosha na pia wamejiandaa kuonyesha 
uwezo.
“Tunawaomba
 wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya 
kutosha kuhakikisha tunashinda. Mchezo huu ni maalum kwa ajiri ya 
kuimalisha Muungano wetu tukufu hivyo tutaendelea kuuenzi na kuukumbatia
 na sote kwa pamoja tuzidishe Amani” alieleza Mh. Mwamotto.
Kwa
 upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji
 Marefu' ambaye ni miongoni mwa viongozi wa msafara wa timu hiyo ya 
Bunge ametamba timu yake kuibuk na ushindi mnono kwani wamejiandaa 
kisaikolojia na mazoezi ya kimichezo.
Naye
 Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
 Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla viongozi wa
 timu hiyo ya Bunge amebainisha kuwa, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa 
majira ya Saa 12 Jioni kesho Aprili 26.2016 katika uwanja huo wa Amani.
“Mechi
 kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza 
la Wawakilishi la Zanzibar. Utachezwa kesho ni siku ya Kuadhimisha 
Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa 
Zanzibar. Tunawaomba watu kujitokeza kwa wingi kuuona mchezo huu ambao 
utakuwa wa aina yake kwa timu zote mbili.” Alieleza DK. Kigwangalla.
Timu
 hiyo ya Bunge yenye wachezaji Zaidi ya 19 imejiandaa vya kutosha katika
 kuakikisha inapata ushindi mnono na ipo Visiwani hapa kwa maandalizi ya
 mchezo huo tokea jana na leo imeweza kufanya mazoezi ya awali asubuhi 
na mengine wakitarajia kufanya hapo jioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni