Waziri
 wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
 Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha bajeti ya ofisi yake wakati wa kikao 
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti 
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es 
Salaam Aprili 12, 2016
Baadhi
 ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya 
kupitisha bajeti wakifuatilia bajeti ya ofisi hiyo walipokutana 
kuijadili na kuipitisha bajeti hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
 Julius Nyerere Dar es Salaam Aprili 12, 2016.
Mkurugenzi
 wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu
 Bw. Issa Nchansi akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu 
ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kupitisha bajeti kilichofanyika tarehe 
12 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar 
es Salaam.
Mwenyekiti
 wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha
 Bajeti Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji (katikati) 
akieleza jambo wakati wa kikao hicho walipokutana kujadili Bajeti ya 
Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 12, 2016 katikaUkumbi wa Mikutano wa Mwalimu
 Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mkurugenzi
 wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya 
(katikati) akifuatilia bajeti ya Idara yake pamoja na wataalamu wake 
kushoto kwake ni Charles Msangi na kulia ni Daniel Alfei wakati wa kikao
 cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti 
Aprili 12, 2016. (Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri wa 
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) 
Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri
 Mkuu kufanya tathimini ya hali halisi za athari zilizosababishwa na 
ndege aina ya kwerea kwerea katika mashamba ya mtama na uwele yaliyopo 
Mkoani Dodoma katika Wilaya Bahi. 
Waziri Mhagama aliyasema hayo 
wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha 
Kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kilichofanyika jana katika 
Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Kikao
 hicho kiliibua hoja za wajumbe ikiwemo hoja iliyo bainisha athari za 
maafa kwa wakazi wa Wilaya ya Bahi kuhusu ukosefu wa chakula baada ya 
mashamba yao kuvamiwa na ndege waharibifu aina ya Kwerea kwerea. 
Hoja
 hiyo iliibuliwa na Mbunge wa Bahi Bw. Omar Badwel alisema wananchi wake
 wapo katika wakati mgumu hivyo wanahitaji msaada kutoka serikalini kwa 
kuwa mazao yao yamevamiwa na ndege hao. 
 “Kwerea kwerea wamekuwa
 ni changamoto kwa wakazi wa wilaya yangu hususani maeneo ya Manyoni 
ninaomba serikali kupitia Idara ya Maafa isaidie kwa kuwapa chakula na 
mbegu Wananchi ili waweze kujikimu na kuitatua changamoto hiyo”Alisema 
Badwel. 
“Mazao yaliyoshambuliwa na kuharibiwa na ndege aina ya kwerea kwerea ni mazao ya mtama na uwele, Alisisitiza”. 
Waziri
 Mhagama alisema anatafuta uwezekano wa kuona umuhimu wa kushirikisha 
Wizara ya kilimo na Mifugo kwa kuangalia namna zinavyoweza kushirikiana 
kuondoa wadudu waharibifu wa mazao mkoani Dodoma. 
“Serikali 
itafanya tathmini kwa waathirika hao wa maafa Wilayani Bahi, ni vizuri 
Idara ya Maafa ifanye hivyo haraka ili kusaidia kunusuru hali ya wakazi 
wa Dodoma”Alisisitiza Mhagama. 
Waziri Mhagama alimpongeza 
Mhe.Badwel kwa kuwajali wananchi wa Bahi kwa kuibua jambo muhimu hivyo 
aliahidi kulitafutia ufumbuzi wa haraka. 
“Suala hili ni muhimu 
kwa kuwa linagusa maisha ya Wananchi moja kwa moja sisi kama  serikali 
tumelichukua kwa uzito na tutahakikisha Idara ya maafa inatembelea 
maeneo husika kwa ajili ya kufanya  tathimini za haraka kwa waathirika 
waliopoteza mazao yao ili kujua namna tunavyoweza kutoa msaada wa haraka
 katika maeneo husika ” alisema Mhagama. 
Awali; kikao hicho 
kililenga kupitia na kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu yenye fungu
 namba 25 (Ofisi Binafsi ya Mhe.Waziri Mkuu), 37(Sera, Uratibu a Bunge),
 15 na 65 (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) na fungu 27 na 61 (Tume
 ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni