Promota wa tamasha la Papa Wemba,
Salif Traore, maarufu kama A'Salfo, amesema Papa Wemba alimuambia
kuwa angependa kufa akiwa jukwaani, katika maongezi yao waliyoyafanya
kwa njia ya simu wiki mbili kabla ya kifo chake.
Papa Wemba mwanamuziki maarufu wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alifariki dunia Jukwaani nchini
Ivory Coast wakati akitumbuiza baada ya kuanguka hafla na kisha
baadaye kuelezwa kuwa amefariki dunia.
Papa Wemba akishambulia jukwaa pamoja na mnenguaji wake kabla ya kuanguka na kufariki dunia
Papa Wemba akionekana mwenye afya njema wakati akitumbuiza
Papa Wemba akifurahi na mashabiki waliokuwa wakishuhudia onyesho hilo ambalo ndio la mwisho kabla ya kuaga dunia
Wanamuziki wa bendi ya Papa Wemba wakiwa wamemzingira baada ya kuanguka chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni