Taifa la Venezuela linatarajia
kuanza mgao wa umeme wa saa nne kwa siku kuanzia wiki ijayo ili
kukabiliana na mgogoro wa nishati ya umeme.
Mgao huo utadumu kwa siku 40 wakati
taifa hilo likihangaika kukabiliana na ukame ulioathiri uzalishaji wa
umeme kwenye mabawa ya umme.
Uchumi wa Venezuela umezidi
kutetereka baada ya bei ya mafuta kushuka thamani na tayari kiwanda
kikuu cha bia cha Polar nchini humo kimetangaza kushindwa kununua
shari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni