Waziri
wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Balozi Augustine Mahiga (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho
kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Pavel Rezac, na kisha
kufanya nae mazungumzo yaliyojikita katika kukuza ushirikiano kati ya
Tanzania na Jamhuri ya Czech.
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule Mhe. Pavel Rezac
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Czech Mhe. Pavel Rezac.
Waziri
wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Balozi Augustine Mahiga (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho
kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Mariano Deng
Ngor, na kisha kufanya nae mazungumzo yaliyojikita katika kukuza
Ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Tanzania na Jamhuri ya
Sudani Kusini.
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule Mhe. Mariano Deng Ngor
Waziri
Mahiga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi
Mteule wa Jamhuri ya Sudani Kusini Mhe. Mariano Deng Ngor (wa tatu
kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Balozi Samwel Shelukindo
(wa kwanza kushoto), Afisa Ubalozi wa Sudani Kusini nchini (wa pili
kutoka kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Eric Ngilangwa (wa kwanza
kulia).
Picha na Reginald Philip.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni