picha
ikionyesha wafanyakazi wa NSSF pamoja na mganga mkuu wa hospitali ya
wilaya ya Tengeru katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada
wa vyandalua
wafanyakazi wa NSSF wakiwa wanabadilishana mawazo nje ya hospitali hiyo
mmoja ya wagonjwa akiwa amekaa kitanda kimoja na watoto wawili wakiwa kila mmoja ana mama yake
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Hospitali ya wilaya ya Tengeru (Patandi) inakabiliwa na ukosefu wa
vitanda hali ambayo inapelekea wagonjwa kulala zaidi ya mmoja katika
kitanda kimoja.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi hili wagonjwa hao mara baada ya kupokea msaada
wa vyandalua kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko wa hifadhi ya jamii
(NSSF) tawi la Arusha walisema kuwa wao kama wagonjwa wa hospitali
hiyo wamekuwa wanapata tabu sana haswa wakati wakiandikiwa kulazwa
kwani wana banana sana na wakati mwingine wanakosa kabisa vitanda.
Mmoja wa wagonjwa hao ambaye alijitambulisha kwa jina la Anna Akyoo
alisema kuwa wamekuwa wakilala wagonjwa wawili hadi watatu hali ambayo
inawafanya wajisikie vibaya kwani wana banana sana katika vitanda
hivyo vichache
Unajua mfano mimi nimekuja hapa unaniona nipo na mtoto wangu lakini
tunalala wawili kwaiyo ukichanganya na watoto wetu maana unaona hii ni
wodi ya mama na mtoto tunakuwa wanne kweli tunaomba sana serekali
ituangalie sana hospitali hii kwani tunateseka nasio kuteseka tu sasa
tunavyobanana hivi muda mungine tunaweza ata kutoka na magonjwa
mengine umu,unakutwa umemleta labda mtoto anaumwa ugonjwa huu tukija
apa huku kubanana badala ya kupona anatoka na gonjwa lingine kweli
watuangalie sana”alisema Lea Mmari
Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali hiyo ya wilaya ya Tengeru
Ukio Kusirigwa alisema kuwa ni kweli tatizo la vitanda lipo lakini sio
kubwa kikubwa kinachowakabili hospitali hiyo ni kukosekana kwa wodi za
kuwalaza wagonjwa hali ambayo inawafanya wawabananishe katika vitanda
hivyo.
“unajua siwezi sema kuwa tatizo la ukosefu wa vitanda hamna hapana
lakini shida kubwa ata tukipata vitanda sasa ivi tutaviweka wapi na
wodi zimeja ,hospitali hii ya wilaya imekuwa inapokea wagonjwa wengi
kutoka tengeru hapa ,mererani na ata kia na kikatiti maana hii ndio
hospitali kubwa ya wilaya iliopo karibu hivyo kwa wingi huo na
ukiangalia wodi ni chache tunakosa jinsi hivyo inatubidi wagonjwa
walale wawili wawili ili waweze kupata huduma”alisema Kusirigwa.
Aidha aliwaomba wadau pamoja na serekali kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi kama vile wafanyakazi wa NSSF tawi la Arusha walivyojitokeza
kuja kutoa misaada angalau ya vitanda,majengo na kikubwa zaidi
aliwaomba sana waisaidie hospitali hiyo kujenga wodi kwa ajili ya
wagonjwa wakiwemo wakina mama na mtoto.
Naye meneja wa NSSF Frank Maduga alisema kuwa wao kama wafanyakazi
wameamua kujichanga na kuweza kusaidia hospitali hii kwa kuwapa
vyandalua hii ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa
malaria.
Alisema kuwa mpaka sasa wameshatoa vyandarua 184 katika hospitali
tofauti ikiwemo ya Mount meru ,St Elizabeth,Levolosi pamoja na kwenye
vituo vya kulelea watoto yatima na wasiojiweza ambacho ni kituo cha
walemavu Usa river na hawataishi hapo tu wao kama wafanyakazi
wamejipanga kila mwisho wa mwezi kutoa msaada katika kila sehemu
ambayo inamlenga mwananchi.
Alitoa kwa wadau mbalimbali kujitoa kwa kuchangia na kusaidia kwa
kutoa misaada katika sehemu mbalimbali ikiwemo watoto yatima ,wasio
jiweza na hata katika hospitali zetu ili kuweza kuwapa moyo wahusika
na sio kusubiri tu serekali ifanye ,kwani kutoa ni moyo ivyo kila mtu
anaeguswa ajitokeze kutoa ikiwemo kuchangia wodi za hospitali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni