MAKUBALIANO YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA KUFIKIWA LEO

Hatua thabiti ya makubaliano ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa inatarajiwa kufikiwa hii leo.

Karibu mataifa 155 yanatarajiwa kusaini rasmi makubaliano katika mkutano wa Umoja wa Mataifa na kuashirika uwezekano wa makubaliano hayo kuanza kutumika mwakani.

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya mataifa yaliyojitokeza kutia saini makubaliano hayo inaonyesha mwamko wa kutaka kubakibiliana na ongezeko la joto duniani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni