WILLIAM RUTO ANGOJEA KUJUA HATMA YA KESI YAKE YA ICC LEO

Makamu wa rais wa Kenya William Ruto anatarajia kubaini kama kesi uhalifu dhidi ya binadamu inayomkabili itaondolewa na Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) watakapotoa uamuzi.

Ruto amekana kuhusika na mashtaka ya mauaji pamoja na kutumia vitisho katika kipindi cha machafuko yalitotokea nchini Kenya baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo watu 1,200 waliuwawa.

Wakili wake anataka kesi hiyo kufutwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi. Ruto ni mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Kenya kushitakiwa mahakama ya ICC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni